
Rais Barrack Obama na wanawe sasha na malia.afisa mmoja wa chama cha Republican amewakosoa mavazi yao.
Watoto wa rais wa Marekani Barrack
Obama,Sasha na Malia wameshtumiwa kwa kukosa heshima na afisa mmoja wa
chama cha Republican baada ya kuhudhuria sherehe za kutoa Shukran.
Elizabeth
Lauten ,ambaye ni mkurugunzi wa mawasiliano wa mbunge Stephen Fincher
alitoa matamshi yake katika mtandao wa facebook ambayo baadaye
yalifutwa.Baada ya kukosolewa Bi Lauten aliomba msamaha kwa kutoa matamshi hayo ya kukera.
Alikua akikosoa skati fupi zilizovaliwa na wasichana hao wa Obama.
Bi Lauteni pia aliwashtumu wasichana hao kwa kuonyesha uchovu wakati waliposimama na baba yao katika sherehe hiyo ya ikulu ya Whitehouse.

''Mama yenu na baba yenu hawaheshimu nyadhfa zao kama inavyohitajika na taifa kwa jumla.
kwa hivyo naona kwamba munakosa ile hadhi ya kuwa kioo cha jamii.Maandishi hayo yaliendelea na kuwashauri wasichana hao kuonyesha kwamba wanaishi katika ikulu ya Whitehouse.
Vaeni mavazi ya kuonyesha munahitaji kuheshimiwa sio kama muko katika baa.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni