Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Ijumaa, 23 Januari 2015

NI SHANGWE BAADA YA VURUGU DRC.


Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kwamba watu 40 wamefariki katika vurugu ingawa serikali imekanusha hilo
Wanaharakati wa upinzani nchini DRC, wanasherehekea kwa kile wanachosema ni ushindi baada ya baraza la Senate kupiga kura kurekebisha mswada uliosababisha vurugu na maandamano kwa siku nne.
Baraza hilo la Senate lilipiga kura kurekebisha mswada huo tatanishi uliopendekeza sheria za uchaguzi kufanyiwa mabadiliko. Limefuta kipengee kinachohitaji kufanyika kwa sensa kote nchini kabla ya uchaguzi kufanyika mwaka ujao.
Mswada huo ndio uliozua vurugu na ghasia katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kwa wiki moja.
Mabadiliko hayo sasa yanafuta kipengee ambacho kingechelewesha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Wapinzani wa Rais Joseph Kabaila wanasema hii ni njama ya Rais kufanya mageuzi ya kikatiba hali ambayo itampa fursa Kabila kusaialia madarakani kwa muhula mwingine.
Kura ya mwisho kuhusu mswada huo itafanyika wiki ijayo katika bunge la waakilishi na baraza hilo la Senate.
Huduma ya internet sasa imerejeshwa nchini humo, katika juhudi za serikali kusitisha vurugu ingawa mitandao ya kijamii bado imevurugwa ili kutatiza mawasiliano.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema zaidi ya watu 40 waliuawa katika vurugu hizo ingawa serikali imepinga madai hayo.
Mkuu wa baraza hilo alitaja uamuzi huo kama wa kihistoria na kusema kuwa masenta walisikiliza kilio cha wengi.
chanzo bbc

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni