
Hassan Rouhani
Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema
nchi yake itatekeleza wajibu wake kikamilifu kuhusiana na muafaka
uliofikiwa kuhusiana na mpango wake wa kupata nguvu za nyuklia mradi tu
wahusika wengine kwenye makubaliano hayo watekeleze wanayopasa
kuyafanya.
Akihutubia taifa hilo kupitia runinga ya nchi hiyo,
rais Rouhani ameongeza kusema mataifa 6 makuu duniani yaliyoshiriki
katika majadiliano hayo walikubali kuwa Iran ina haki ya kuendelea na
mpango huo ndani ya mipaka yake na bila kuhatarisha usalama wa mataifa
mengine.Chini ya makubaliano hayo Iran imekubali kupunguza kiwango cha mradi huo kwa zaidi ya theluthi mbili.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni