
Mazoezi ya kijeshi ya mwaka daima yamekuwa yakisababisha uhasama katika peninsula ya Korea.
Korea Kaskazini imefyatua makombora
mawili ya masafa mafupi katika bahari wakati mazoezi ya pamoja ya
kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini yakiendelea.
Makombora
hayo mawili yakiruka katika masafa ya kilomita 490, yalifyatuliwa
kuelekea baharini kutoka mji wa magharibi wa Nampo, limesema jeshi la
Korea Kusini.Mazoezi, yanayohusisha maelfu ya askari daima yamekuwa yakiiudhi Korea Kaskazini.
Korea Kusini na Marekani zinaelezea mazoezi hayo ya kijeshi kuwa yana lengo la kujihami. Korea Kaskazini inayaita mazoezi hayo kuwa yana lengo la uvamizi.
Korea Kaskazini imefanya majaribio ya nyuklia katika mwaka 2006, 2009 na 2013. Mazungumzo ya mataifa sita yanayolenga kumaliza mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini yamekwama tangu mapema mwaka 2009.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni