Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumanne, 21 Oktoba 2014

MTOTO WA MIEZI MINNE AMPONZA KUAGA MASHINDANO YA BIG BROTHER


Baada tu ya wiki mbili katika nyumba ya Big Brother Mwakilishi mmoja wa Kenya Sabina ametimuliwa.

Sabina ana mtoto wa miezi minane na ndio mkenya wa kwanza kutimuliwa kutoka katika nyumba hiyo.

Inadaiwa kuwa watazamaji na mashabiki wa makala hiyo waliamua kumuondoa Sabina baada ya siku 14 pekee ili aende kumuhudumia mwanawe.

Sabina alionekana kumkosa sana mwanawe na wakati mwingi alionekana akifunga vitu kwenye mgongo wake ungedhani anambeba mtoto.

Sabina alionekana kuwa kipenzi cha wengi

Aliweka pamoja blanketi na nguo na kuvifunga kwenye mgo wake akiwa na kofia ya mwanawe huku akitembea katika nyumba hiyo kabla ya kujiunga na wenzake waliokuwa wakijivinjari nje.

Baadhi wanasema kufunga vitu mgongoni ndio chanzo za mashabiki kuanza kuomuonea huruma Sabina wakisema bora aende nyumbani kwa mwanawe mwenye miezi minane.

Na hapo ndipo walipompigia kura Jumapili na kumtimua kutoka katika Big Brother house.

Sabina alitimuliwa kutoka katika nyumba hiyo pamoja na Lilian kutoka Nigeria na Esther wa Uganda.

Hatua ya kumondoa Sabina katika Big Brother house inamwacha mwakili mmoj tu wa Kenya Melvin Alusa ambaye ni kakake Ben aime Baraza wa kikundi cha wanamuziki cha Sauti Sol.



UCHAWI WAMPONZA MREMBO NIGERIA

Maajabu ya Ndege kugeuka mtu Nigeria


Mmoja wa waliomuangushia kichapo mwanamke huyo hadi akafariki

Kisa cha kushangaza kilitokea nchini Nigeria ambapo mwanamke mmoja alipewa kichapo cha mbwa hadi akafariki kwa madai ya yeye kuwa mchawi.

Mwanamke huyo inasemekana alikuwa Ndege iliyokuwa inaruka mtini kabla ya kugeuka na kuwa binadamu.

Umati wa watu ulikusanyika eneo alilokuwa mwanamke huyo baahi wakinasa matukio kwenye simu zao za mkononi. Polisi wawili walilazimika kurusha mabomu ya petroli kuwatawanya watu hao na kuwazuia kunasa picha za mwanamke huyo aliyekuwa anachapwa sana.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, mmoja alisema kuwa mwanamke huyo dakika chache zilizopita alikuwa Ndege mtini kabla ya kugeuka na kuwa mwanamke.

Ndege huyo alikuwa anazunguka mti mjini Oshodi , kisha akagonga mlingoti wa stima kabla ya kuanguka ardhini ambapo aligeuka na kuwa mwanamke.

Hii ni kwa mujibu wa wakazi wa mjini Oshodi wanaodai kuwa mwanamke huyo alikuwa mchawi.

'Kitu cha kushangaza'

''Ni kitu cha kushangaza lakini ni cha kweli,'' alisema bwana Sobowale.

"tulipozungumza na mwanamke huyo alidai kuwa na nguvu za kiganga, na kwamba alikuwa amewaua watu kadhaa. Aliongeza kuwa alikuwa anarejea kwa mumewe anayeishi katika eneo la Mushin kabla ya tyukio hilo. Baadhi ya watu walianza kumpiga picha. ''

Video ya umati huo ukimtandika mwanamke huyo imeenea kama moto msituni na kutazamwa na maelfu ya watu kwenye mtandao wa kijamii wa YouTube.

Mwanamke huyo alikuwa uchi wa mnyama huku ngozi yake ikiwa inatoka baada ya kuchomwa.

Polisi hawajuzungumzia tukio hilo, hususan kabla ya umati huo kukusanyika na kuanza kumchapa mwanamke huyo.

Alifariki mda mfupi baadaye huku mwili wake ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu.



Jumatatu, 13 Oktoba 2014

MWANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU WA MWAKA WA KWANZA AJICHOMA KISU.

Mwanafunzi aliefahamika kwa jina moja la Moza alie mwaka
wa kwanza katika chuo cha Uhasibu TIA Mkoani Singida
amenusurika kufa baada ya jaribio la kutaka kujiua kwa
kujichoma na kisu kushindikana,tukio hilo limetokea jana
baada mwanafunzi huyo kumfumania mpenzi wake wa kiume
akiwa na mwanamke mwingine.

Ijumaa, 10 Oktoba 2014

WATU 9 WAFARIKI KWA AJALI YA BOTI 30 HAWAJULIKANI WALIPO

Ajali ya boti yauwa 9 Guinea, 30 hawajulikani walipo

Kiasi ya watu wa tisa wamekufa na wengine 30 kutojulikana walipo kutokana na ajali ya boti iliyotokea kwenye mto Guinea. Kwa mujibu wa taarifa ya wakazi na polisi katika eneo hilo, ajali hiyo imetokea jana alasiri karibu na mji wa Contaah, wilaya ya Forecariah, iliyopo umbali wa kilometa 100 kusini/mashariki mwa Conakry. Mkazi wa Forecariah alililithibitishia shirika la habari la Uingereza Reuters kutokea kwa mkasa huo.  Matukio ya ajali za boti katika eneo la Afrika Magharibi yamekuwa kama ya kawaida kutokana na kutotimizwa taratibu za usafiri salama na hasa katika maeneo ya karibu na Forecariah ambako kumekuwa na vijiji kadhaa vilivyo karibu na visiwa.


JUMUIYA YA KIMATAIFA IMEPOKEA VYEMA USHINDI WA TUZO YA NOBEL

Pongezi kwa washindi wa Tuzo ya Nobeli

Jumuiya ya kimataifa imepokea vyema ushindi wa Tuzo ya Nobeli kwa msichana Malala Yousafzai wa  Pakistani na Kailish Satyarthn wa Iindia. Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amenukuliwa akisema " Hii ni siku nzuri kwa watoto duniani. Watoto ambao hivi leo hawana haki ya utoto wao, elimu, kutokiukwa utu wao, wamepata sauti zao za haki ya elimu na kupinga utumikishwaji wa ajira usiyo wa haki kupitia wawakilishi hao wawili walioshinda tuzo. Nao marais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso na wa Baraza la umoja huo Herman Van Rompuy walitoa taarifa ya pamoja wakisema " Hatuwezi kuwasahau mamilioni ya watoto duniani kote ambao wananyimwa haki yao ya kupata elimu". Na kuongeza kusema huo ni ushindwa kwa wote.


EBOLA ITATUMALIZA

Idadi ya waliokufa kwa Ebola yapindukia 4,000 Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema jana kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana ugonjwa wa Ebola imepindukia 4,000, huku muuguzi wa Madrid akipigania kunusuru maisha yake na serikali duniani kote zikijaribu kudhibiti hofu kutokana na ugonjwa huo hatari. WHO imesema watu 4,033 wamekufa kutokana na ugonjwa huo kufikia Oktoba 8. Idadi hiyo ni miongoni mwa visa rasmi 8,399 vilivyobainika katika mataifa saba tofauti. Ongezeko kubwa la vifo limekuja wakati Umoja wa Mataifa ukisema ahadi za kukabiliana na mripuko huo zimeshuka chini ya kiasi cha dola bilioni moja zinazohitajika kukabilaiana na mripuko huo. Mbali na Magharibi ya Afrika, ambako idadi kubwa ya vifo imetokea, mashaka yameongezeka katika maeneo mengine. Kuanzia Australia hadi Zimbabwe, na Macedonia  hadi Uhispania, watu walioonyesha dalili za homa au walikuwa na mawasiliano na waathirika wa Ebola wamewekwa katika maeneo yaliyotengwa au wameamriwa kubakia majumbani mwao.

FAMILIA YA BABA WA TAIFA WAIOMBA BENKI KUU KUONDOA NOTI YA SHILINGI ELFU MOJA

Familia ya Baba wa Taifa waiomba benki kuu ya Tanzania kuondoa noti ya shilingi elfu moja.

Familia ya baba wa taifa hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere imeuomba uongozi wa benki kuu ya Tanzania kuiondoa katika  mzunguko wa fedha noti ya shilingi elfu moja yenye picha ya Baba kwa maelezo kuwa picha ambayo imetumika katika noti hiyo haifanani kabisha na kiongozi huyo na kwamba kuendelea kutumika ni sawa na kumdhalilisha muasisi huyo wa taifa la Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya familia na ukoo wa Baba wa taifa wakati wa kupokea mradi wa kuboresha makumbusha ya Mwalimu Nyerere na kuzindua onesho la noti na sarafu ambazo zimetumika katika vipindi tofauti kuanzia mwaka 1967 hadi sasa zenye picha na sahihi ya Baba wa taifa, mmoja wa watoto wa Baba wa taifa Bw Madaraka Nyerere, amesema picha iliyopo katika noti hiyo ya shilingi elfu moja haifanani na sura ya kiongozi huyo hivyo kuomba benki hiyo kuangalia uwezekano wa kuiondoka katika mzunguko.



Naye kaimu gavana wa benki kuu ya Tanzania Bw Juma Reli, pamoja na kutoa ahadi ya ukarabati nyumba ya kwanza ya Baba wa taifa ambayo aliitumia kabla ya kujengewa na tanu amesema kuwa benki hiyo imejitolea kuboresha makumbusho hayo ili kuhifadhia kumbukumbu zenye histori ya baba wa taifa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.



Kwa upande wao mkurugenzi mkuu wa shirika la makumbusho ya taifa Profesa Audax  Mabula na mkuu wa wilaya ya butiama Bi Angelina  Mabula, wameishukuru benki kuu ya Tanzania kwa kutambua umuhimu wa kuboresha makumbusho hayo katika kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere ili kulinda historia za kiongozi huyo.


ASKARI WATATU WA USALAMA BARABARANI WAFUKUZWA KAZI

Jeshi la Polisi limewafukuza kazi askari watatu kwa utovu wa nidhamu mkoani Kagera.

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewafukuza kazi askari watatu wenye vyeo na nafasi mbalimbali katika jeshi hilo kutokana na utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili mema kazini.

Akiongea mjini Bukoba kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Kagera Henri Mwaibambe amesema askari hao walipiga picha mbaya na kuziweka kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kwamba picha hiyo walipiga kinyume na maadili ya jeshi la Polisi ambapo ameongeza kuwa picha hiyo walipiga wakiwa kazini.

Kamanda Mwaibambe amewataja kwamajina askari wote waliofukuzwa kazi kuwa Mpaji Asuma Mwasumbi, Fadhili Linga, Veronika Nazaremo   wote walikuwa askari wa usalama barabarani.

Aidha kamanda Mwaibambe amesema maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari wote wanafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polisi lakini kwa kitendo walichokifanya jeshi hilo limeamua kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi ili liwefundisho kwa askari wengine.




Alhamisi, 9 Oktoba 2014

RAIS UHURU KENYATTA APOKELEWA KWA SHANGWE NA VIGELEGELE AKITOKEA KATIKA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA ICC MJINI THE HAGUE.


Mamia ya watu kwa shangwe na vigelegele wamemkaribisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kurejea kutoka kikao chake katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini the Hague.

Kenyatta alihudhuria kikao maalum katika mahakama hiyo Jumatano, na kuwa Rais wa kwanza aliye mamlakani kufika katika mahakama hiyo.

Mahakama hiyo ilimtaka afike mbele yake kutokana na malalalmsihi kutoak kwa kiongozi w amashitkaka kuwa serikali ya Kenya inaficha ushahihidi kuhusiana na kesi

Alikanusha madai ya uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 ambayo yalisababisha vifo vya watu 1,200 na kuwaacha wengine zaidi ya laki sita bila makao.

Kenyatta alipokelewa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanacheza densi pamoja na gwaridde la heshima.

Asubuhi na mapema, wafuasi wake walipanga foleni kwenye barabara ya kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Nairobi.

Walipeperusha bendera na kusikika wakiimbia kwa shangwe na kumsifgu Kenyatta wakisema kuwa Rais wao hana hatia.

Rais aliwahutubia kwa mda mfupi umati huo wa watu ambao waliombwa kufika kumpokea rais na waziri wa usalama.



KIAZI CHAOTA KWENYE MWILI WA MWANAMKE


Kiazi kilipatikana kikimea ndani ya kizazi cha mwili wa mwanamke mmoja baada ya kujaribu kukitumia kama kifaa cha kuzuia mimba.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 22 kutoka nchini Colombia ambaye jina lake halikutajwa alijaribu kutumia kiazi hicho ili kuzuia mimba na alipomtembelea daktari baada ya kulalamika kuhusu maumivu ya tumbo ,iligunduliwa kuwa kiazi hicho kilikuwa kimeota mizizi ambayo ilianza kumea ndani ya kizazi chake.

Kulingana na Gazeti la Nation nchini kenya msichana huyo amedai kuwa mamaake alimshauri kwamba iwapo angependelea kuzuia mimba basi alifaa kuweka kiazi ndani ya kizazi chake.

Licha ya hatari aliyokumbana nayo mwanamke huyo hakuathirika huku kiazi hicho kikitolewa bila kufanyiwa upasuaji.
Epuka njia zisizo rasmi za kuzuia mimba.

Microsoft yazindua Windows 10
Kampuni ya Microsoft imezindua programu mpya ya Windows 10 ambayo imeipiku Windows 9.

Kampuni hiyo pia inatarajia wateja wake watarudi kwani wengi walikuwa wakisitasita kuboresha oparesheni zao tangu Windows 8.

Windows 10 itaingiliana na vifaa vingi hususan kutokana na uwezo wake wa kubadilisha ukubwa wa programu yake.

Kwa taarifa hii na nyenginezo za teknologia endelea kutembelea blogs hii



Leo tutajifunza kwa undani sifa kumi za mpenzi bora ili tuweze kuwatambua wapenzi wetu
kabla ya kuwapa mioyo na utu wetu .

1. Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.Kwa kuwa ana mapenzi ya dhati na anajua mahitaji yako , hawezi kusubiri kushurutishwa au ionekane kama vile anatoa hongo . Kipengele hiki kinawahusu wanaume zaidi .
2. Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .Hata kama ukiwa huna furaha , hujiona mwenye jukumu kuhakikisha unakuwa nayo kwa namna yoyote ile .
3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatajali umezungumza baya au zuri . Kwa bahati nzuri ni kwamba , ikiwa umekosea , yeye atachukua jukumu la kukuweka sawa.
Asiye na penzi la dhati, ukikosea kwake ni kichekesho . Badala ya kukurekebisha na kukuweka kwenye mstari, atakucheka .
4. Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha . Hatakuwa mtu wa kuviziavizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha . Kwake, shida yako itakuwa yake akiwa na imani kuwa , hata yake ni yako pia. Anayejiweka kando ukiwa na matatizo , siyo sahihi, mwepuke .
5. Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatapenda kuwa kikwazo cha maisha yako , atakulinda daima.Heshima ni msingi mkuu.
6. Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani . Pesa si kipaumbele chake.
7. Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine , hafichi hisia zake mbele za watu , atakutetea na kukufanya wa kwanza .
8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.
9. Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini , asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya
maamuzi magumu. Kikubwa ni kusimamia katika ukweli na masilahi yanayoeleweka .
10. Atakuwa tayari kuvumilia , hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe . Nimwelekezaji zaidi , hawezi kukurushia maneno ya kuudhi maana anajua kukuudhi au kukuumiza ni kuharibu maana nzima ya penzi lenu
Mc.Ray
0659/375263.

Jumanne, 7 Oktoba 2014

TAMBUA WAJIBU WA MUME NA MKE KATIKA MAISHA YA NDOA




WAJIBU WA MUME NA MKE KATIKA MAISHA YA NDOA.

Swali: "Majukumu ya mume na mke ni gani katika familia?"

Jibu: Ingawa wanaume na wanawake wako sawa katika uhusiano na Kristo, maandiko yanatoa majukumu maalum kwa kila mmoja katika ndoa. Mume anapaswa kuchukua uongozi katika boma (1 Wakorintho 11:3, Waefeso 5:23). Uongozi huu usiwe wa kihimla, kukandamisa, au shupavu kwa mke, lakini lazima iwe kwa mujibu wa mfano wa Kristo kuongoza kanisa. "Enyi wanaume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neon" (Waefeso 5:25-26). Kristo alivyolipenda kanisa (watu wake) na huruma, rehema, msamaha, heshima, na kutokuwa na ubinafsi. Kwa njia hiyo waume wanapaswa kuwapenda wake zao.

Wake wanapaswa kunyenyekea kwa mamlaka ya waume zao. "Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa, naye ni mwokozi wa mwili wake. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo" (Waefeso 5:22-24). Ingawa wanawake wanapaswa kunyenyekea kwa waume zao, Biblia pia anawaambia wanaume mara kadhaa jinsi wanatakiwa kuwafanyia wake zao. Mume hapaswi kuchukua nafasi ya kiihimla, lakini wanapaswa kuonyesha heshima kwa mke wake na maoni yake. Kwa kweli, Waefeso 5:28-29 anawahimiza watu kuwapenda wake zao katika njia sawa wanavyoipenda miili yao wenyewe, kuwalisha na kuwatunza. Upendo wa mume kwa mke wake unapaswa kuwa sawa na upendo wa Kristo kwa mwili wake, kanisa.

"Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. Ninyi Waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao "(Wakolosai 3:18-19). "Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpamke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe" (1 Petro 3: 7). Kutokana na mistari hii tunaona kwamba upendo na heshima ni sifa ya majukumu ya waume wote na wake. Kama haya yapo katika ndoa, basi mamlaka, uongozi, upendo, na kunyenyekea hakutakuwa na tatizo kwa mpenzi yeyote.

Kuhusiana na suala la mgao wa majukumu katika boma, Biblia inawaamuru waume kukimu familia zao. Hii ina maana kuwa anafanya kazi na kupata fedha za kutosha kukimu mahitaji yote ya maisha kwa mke na watoto wake. Kwa kushindwa kufanya hivyo ina madhara maalum ya kiroho. "Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani wale wa numbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini" (1 Timotheo 5:8). Hivyo, mume ambaye hafanyi juhudi za kukimu mahitaji ya familia yake haiwezi kujiita Mkristo halisi. Hii haimaanishi kwamba mke hawezi eza katika kusaidia familia Mithali 31 inaonyesha kuwa mke mcha Mungu anaweza hakika kufanya hivyo-lakini kukimi familia si hasa wajibu wake; ni wa mume wake. Wakati mume anasaidia kutayarisha watoto na kufanya kazi za nyumbani (hivyo kutimiza wajibu wake wa kumpenda mke wake), Mithali 31 pia inaweka wazi kwamba nyumbani ni eneo kimsingi mwanamke ushawishi na wajibu. Hata kama yeye ni atalazimika kulala akiwa amechelewa na kuamka mapema, familia yake imetunzwa vyema. Haya sio maisha rahisi kwa wanawake wengi hasa katika mataifa tajiri ya Magharibi. Hata hivyo, wanawake wengi mno wamesumbuliwa na kusukumwa hadi kiwango cha talaka. Ili kuzuia matatizo hayo, wote wawili mume na mke wanapaswa kimaombi kupanga tena vipaumbele vyao na kufuata maelekezo ya Biblia juu ya majukumu yao.

Migogoro kuhusu mgao wa kazi katika ndoa hakika hutokea, lakini endapo wapenzi wote wawili ni wanyenyekevu kwa Kristo, migogoro hii itakuwa ndogo. Kama wanandoa hupata mapishano juu ya suala hili mara kwa mara na wakali, au kama mapishano yanaonekana kuwa tabia ya ndoa, tatizo ni la kiroho. Katika hali hiyo, washirika lazima wawe na juhudi wenyewe kwa maombi na kunyenyekea kwa Kristo kwanza, basi kwa mtu mwingine katika mtazamo wa upendo na heshima.
mc,Ray
0659/375263


Jumatatu, 6 Oktoba 2014




KWA WALE WASIOJUA MAANA YA NDOA WASOME HAPA

NDOA NINI ???
Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda
wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).
i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.
ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.
iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.
Mpango na utaratibu wa MUNGU kwa wanandoa umewekwa wazi katika kitabu cha Mwanzo.
“Bwana MUNGU akasema si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufafana
naye”. Mwanzo 2:18.
Hapa tunaona kuna suala la mamlaka katika ndoa, kwamba mke ni msaidizi.
“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao
watakuwa mwili mmoja”. Mwanzo 2:24.
Hapa tunaona kusudi la MUNGU katika suala la kuachana na kuambatana. Wanandoa wanatakiwa
kuachana na wazazi wao katika maeneo matatu.
i) Kimwili – wawe na makazi yao wenyewe
ii) Kihisia – wategemeane na kutiana moyo na kusaidiana
iii) Kiuchumi – wajitegemee kwa mahitaji yao ya kila siku.
TENDO LA NDOA
Ukizingatia kanuni za MUNGU kibiblia kuhusu tendo la ndoa kwa wanandoa;-
i) Ni tukio dogo lenye umuhimu mkubwa.
ii) Kusudi kubwa la tendo la ndoa ni uzazi.
iii) Ni kinga dhidi ya majaribu.
iv) Ni burudani/starehe.
v) Ni suala la kuwa na uvumilivvu na kujitoa.
NDOA -TAASISI TAKATIFU
Ndoa yenye furaha na kuheshimika ni ile ambayo kila mmoja anafahamu na kutimiza wajibu wake
katika ndoa kwa mujibu wa nafasi yake. Na hii ndio sharti la msingi kutupelekea kwenye ndoa
yenye mafanikio.
i) Kumheshimu mwenzi wako kutokana na hadhi aliyonayo kama MUNGU alivyoagiza.
ii) Heshima inasaidia kutuepusha na ubinafsi na kuongozwa na hisia.
iii) Heshima katika ndoa inachochea mapenzi.
NDOA NI KUTOA
1. Ndio sio mkataba wa kijamii bali agano la kiroho. Waefeso 5:31-33 Kwa sababu hiyo mtu
atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili
mmoja. Siri hiyo ni kubwa, ila mimi nanena habari ya KRISTO na Kanisa. Lakini kila mtu ampende
mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose kumstahi mumewe.
Hapa tunajifunza
i) Ndoa ni fumbo la ajabu la kiroho linalowaunganisha watu wawili, mwanamume na mwanamke
(mst.31)
ii) Ndoa ya kikristo inaliganishwa na uhusiano uliopo kati ya KRISTO na Kanisa (mst.32)
iii) Mpango wa MUNGU katika ndoa unahitaji upendo wa kujitoa sadaka kama KRISTO
anavyofanya kwa Kanisa (mst.33)
2. Ndoa ya Kikristo ni kujitoa sio kupokea. Wafilipi 2:3-4 Msitende neno lolote kwa kushindana
wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenzie kuwa bora kuliko nafsi
yake mwenyewe. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya
wengine.
Hapa tunajifunza
i) Kutokuwa wabinafsi
ii) Unyenyekevu
iii) Roho ya kutoa na kujitoa.
Wewe mume/mke, mahusiano yako na mwenzi wako yakoje? Unampenda mwenzi wako kama
KRISTO anavyolipenda Kanisa lake? Kama wewe ni mmojawapo wa wasiofuata kielelezo cha
KRISTO katika ndoa usijisikie vibaya kwani hakuna aliye mkamilifu. Hata hivyo wajibu huu
haukwepeki kwani ni agizo la MUNGU na lazima kutii maagizo yake, kumpenda MUNGU kwa moyo
waklo wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. Na kumpenda
jirani yako kama nafsi yao. Marko 12:30-31. Hivyo, hii ni nafasi yako ya kumwonyesha mwenzi
wako upendo ambao wa muda mrefu ameukosa, upendo ambao KRISTO ameuonyesa kwa kanisa lake.
Mc,Ray
0659/375263

Jumapili, 5 Oktoba 2014



YES IDO.....Nkipindi kipya cha TV, Kipindi kinachoelezea ndoa na wanandoa,kipindi hiki ni cha dk 30,kipindi kitakachokuwa kinaluka kila Jumamosi saa kumi na moja jioni na marudio jumapili saa kumi na moja hiyohiyo.
Kipindi hiki kimegawanyika katika sehemu kuu mbili.

  1. Sehemu hii ya kwanza kinahusu mahojiano ya wanandoa juu ya maisha ya ndoa hapa utaweza kusikia changamoto mbambali zinazo wakumba wanandoa katika maisha ya ndoa,vilele katika sehemu hii ya kwanza utaweza kumsikia mshauri au mwl akitufundisha masomo ya ndoa na jinsi gani tunavyoweza kuoambana na changamoto na hata kutatua matatizo yanayotukabili katika maisha ya ndoa,nakama utakuwa na tatizo binafsi ataweza kukutatulia tatizo lako kwa utaratibu mzuri uliowekwa.
  2. sehemu hii ya pili utaweza kuona baadhi ya harusi kitchen party,na hata send off.pia utaweza kusikia ushauri jinsi ya kuipendezesha shughuli yako kutoka kwa wataalamu  mbalimbali mfano wataalamu wa mapambo,mavazi,mapishi mziki nk,
Kipindi hiki kitakuwa kinawalenga:-
wanandoa na wale wanaoingia katika maisha ya ndoa.
Dhumuni la kipindi:-
  • Kuwaweka wanandoa pamoja
  • kutatua migogoro ya ndoa 
  • ushauri jinsi ya kuipendezesha shughuli ya harusi,send off,na hata kitchen party.
  • kuwapatanisha wanandoa walio tengana.
Mtayarishaji wa Kipindi hiki ni Raymond Mushi.
          kitaonekana Tv gani endelea kutembelea bligspot hii kwa taarifa zaidi.