Jeshi la Polisi limewafukuza kazi askari watatu kwa utovu wa nidhamu mkoani Kagera.
Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewafukuza kazi askari watatu wenye vyeo na nafasi mbalimbali katika jeshi hilo kutokana na utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili mema kazini.
Akiongea mjini Bukoba kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Kagera Henri Mwaibambe amesema askari hao walipiga picha mbaya na kuziweka kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kwamba picha hiyo walipiga kinyume na maadili ya jeshi la Polisi ambapo ameongeza kuwa picha hiyo walipiga wakiwa kazini.
Kamanda Mwaibambe amewataja kwamajina askari wote waliofukuzwa kazi kuwa Mpaji Asuma Mwasumbi, Fadhili Linga, Veronika Nazaremo wote walikuwa askari wa usalama barabarani.
Aidha kamanda Mwaibambe amesema maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari wote wanafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polisi lakini kwa kitendo walichokifanya jeshi hilo limeamua kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi ili liwefundisho kwa askari wengine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni