Shule
![Shule](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhowosffr85R15Iy8OeXGODZp5kd2v0ncDhKEPBKYhYhAU1s6Cjj7sf6d6qCwYkz-nRr7mMc1AtErm869z7-WhD5IUWXoPH-MEepRv9S3MAMZ_7sKHSvmJEdFmwxh2vFgslpN7fTH_kULGM/s1600/Tangazo.jpg)
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache
Alhamisi, 9 Oktoba 2014
Leo tutajifunza kwa undani sifa kumi za mpenzi bora ili tuweze kuwatambua wapenzi wetu
kabla ya kuwapa mioyo na utu wetu .
1. Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.Kwa kuwa ana mapenzi ya dhati na anajua mahitaji yako , hawezi kusubiri kushurutishwa au ionekane kama vile anatoa hongo . Kipengele hiki kinawahusu wanaume zaidi .
2. Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .Hata kama ukiwa huna furaha , hujiona mwenye jukumu kuhakikisha unakuwa nayo kwa namna yoyote ile .
3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatajali umezungumza baya au zuri . Kwa bahati nzuri ni kwamba , ikiwa umekosea , yeye atachukua jukumu la kukuweka sawa.
Asiye na penzi la dhati, ukikosea kwake ni kichekesho . Badala ya kukurekebisha na kukuweka kwenye mstari, atakucheka .
4. Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha . Hatakuwa mtu wa kuviziavizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha . Kwake, shida yako itakuwa yake akiwa na imani kuwa , hata yake ni yako pia. Anayejiweka kando ukiwa na matatizo , siyo sahihi, mwepuke .
5. Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatapenda kuwa kikwazo cha maisha yako , atakulinda daima.Heshima ni msingi mkuu.
6. Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani . Pesa si kipaumbele chake.
7. Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine , hafichi hisia zake mbele za watu , atakutetea na kukufanya wa kwanza .
8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.
9. Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini , asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya
maamuzi magumu. Kikubwa ni kusimamia katika ukweli na masilahi yanayoeleweka .
10. Atakuwa tayari kuvumilia , hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe . Nimwelekezaji zaidi , hawezi kukurushia maneno ya kuudhi maana anajua kukuudhi au kukuumiza ni kuharibu maana nzima ya penzi lenu
Mc.Ray
0659/375263.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni