YES IDO.....Nkipindi kipya cha TV, Kipindi kinachoelezea ndoa na wanandoa,kipindi hiki ni cha dk 30,kipindi kitakachokuwa kinaluka kila Jumamosi saa kumi na moja jioni na marudio jumapili saa kumi na moja hiyohiyo.
Kipindi hiki kimegawanyika katika sehemu kuu mbili.
- Sehemu hii ya kwanza kinahusu mahojiano ya wanandoa juu ya maisha ya ndoa hapa utaweza kusikia changamoto mbambali zinazo wakumba wanandoa katika maisha ya ndoa,vilele katika sehemu hii ya kwanza utaweza kumsikia mshauri au mwl akitufundisha masomo ya ndoa na jinsi gani tunavyoweza kuoambana na changamoto na hata kutatua matatizo yanayotukabili katika maisha ya ndoa,nakama utakuwa na tatizo binafsi ataweza kukutatulia tatizo lako kwa utaratibu mzuri uliowekwa.
- sehemu hii ya pili utaweza kuona baadhi ya harusi kitchen party,na hata send off.pia utaweza kusikia ushauri jinsi ya kuipendezesha shughuli yako kutoka kwa wataalamu mbalimbali mfano wataalamu wa mapambo,mavazi,mapishi mziki nk,
wanandoa na wale wanaoingia katika maisha ya ndoa.
Dhumuni la kipindi:-
- Kuwaweka wanandoa pamoja
- kutatua migogoro ya ndoa
- ushauri jinsi ya kuipendezesha shughuli ya harusi,send off,na hata kitchen party.
- kuwapatanisha wanandoa walio tengana.
kitaonekana Tv gani endelea kutembelea bligspot hii kwa taarifa zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni