Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Ijumaa, 10 Oktoba 2014

EBOLA ITATUMALIZA

Idadi ya waliokufa kwa Ebola yapindukia 4,000 Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema jana kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana ugonjwa wa Ebola imepindukia 4,000, huku muuguzi wa Madrid akipigania kunusuru maisha yake na serikali duniani kote zikijaribu kudhibiti hofu kutokana na ugonjwa huo hatari. WHO imesema watu 4,033 wamekufa kutokana na ugonjwa huo kufikia Oktoba 8. Idadi hiyo ni miongoni mwa visa rasmi 8,399 vilivyobainika katika mataifa saba tofauti. Ongezeko kubwa la vifo limekuja wakati Umoja wa Mataifa ukisema ahadi za kukabiliana na mripuko huo zimeshuka chini ya kiasi cha dola bilioni moja zinazohitajika kukabilaiana na mripuko huo. Mbali na Magharibi ya Afrika, ambako idadi kubwa ya vifo imetokea, mashaka yameongezeka katika maeneo mengine. Kuanzia Australia hadi Zimbabwe, na Macedonia  hadi Uhispania, watu walioonyesha dalili za homa au walikuwa na mawasiliano na waathirika wa Ebola wamewekwa katika maeneo yaliyotengwa au wameamriwa kubakia majumbani mwao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni