Shule
![Shule](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhowosffr85R15Iy8OeXGODZp5kd2v0ncDhKEPBKYhYhAU1s6Cjj7sf6d6qCwYkz-nRr7mMc1AtErm869z7-WhD5IUWXoPH-MEepRv9S3MAMZ_7sKHSvmJEdFmwxh2vFgslpN7fTH_kULGM/s1600/Tangazo.jpg)
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache
Jumatatu, 6 Oktoba 2014
KWA WALE WASIOJUA MAANA YA NDOA WASOME HAPA
NDOA NINI ???
Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda
wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).
i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.
ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.
iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.
Mpango na utaratibu wa MUNGU kwa wanandoa umewekwa wazi katika kitabu cha Mwanzo.
“Bwana MUNGU akasema si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufafana
naye”. Mwanzo 2:18.
Hapa tunaona kuna suala la mamlaka katika ndoa, kwamba mke ni msaidizi.
“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao
watakuwa mwili mmoja”. Mwanzo 2:24.
Hapa tunaona kusudi la MUNGU katika suala la kuachana na kuambatana. Wanandoa wanatakiwa
kuachana na wazazi wao katika maeneo matatu.
i) Kimwili – wawe na makazi yao wenyewe
ii) Kihisia – wategemeane na kutiana moyo na kusaidiana
iii) Kiuchumi – wajitegemee kwa mahitaji yao ya kila siku.
TENDO LA NDOA
Ukizingatia kanuni za MUNGU kibiblia kuhusu tendo la ndoa kwa wanandoa;-
i) Ni tukio dogo lenye umuhimu mkubwa.
ii) Kusudi kubwa la tendo la ndoa ni uzazi.
iii) Ni kinga dhidi ya majaribu.
iv) Ni burudani/starehe.
v) Ni suala la kuwa na uvumilivvu na kujitoa.
NDOA -TAASISI TAKATIFU
Ndoa yenye furaha na kuheshimika ni ile ambayo kila mmoja anafahamu na kutimiza wajibu wake
katika ndoa kwa mujibu wa nafasi yake. Na hii ndio sharti la msingi kutupelekea kwenye ndoa
yenye mafanikio.
i) Kumheshimu mwenzi wako kutokana na hadhi aliyonayo kama MUNGU alivyoagiza.
ii) Heshima inasaidia kutuepusha na ubinafsi na kuongozwa na hisia.
iii) Heshima katika ndoa inachochea mapenzi.
NDOA NI KUTOA
1. Ndio sio mkataba wa kijamii bali agano la kiroho. Waefeso 5:31-33 Kwa sababu hiyo mtu
atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili
mmoja. Siri hiyo ni kubwa, ila mimi nanena habari ya KRISTO na Kanisa. Lakini kila mtu ampende
mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose kumstahi mumewe.
Hapa tunajifunza
i) Ndoa ni fumbo la ajabu la kiroho linalowaunganisha watu wawili, mwanamume na mwanamke
(mst.31)
ii) Ndoa ya kikristo inaliganishwa na uhusiano uliopo kati ya KRISTO na Kanisa (mst.32)
iii) Mpango wa MUNGU katika ndoa unahitaji upendo wa kujitoa sadaka kama KRISTO
anavyofanya kwa Kanisa (mst.33)
2. Ndoa ya Kikristo ni kujitoa sio kupokea. Wafilipi 2:3-4 Msitende neno lolote kwa kushindana
wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenzie kuwa bora kuliko nafsi
yake mwenyewe. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya
wengine.
Hapa tunajifunza
i) Kutokuwa wabinafsi
ii) Unyenyekevu
iii) Roho ya kutoa na kujitoa.
Wewe mume/mke, mahusiano yako na mwenzi wako yakoje? Unampenda mwenzi wako kama
KRISTO anavyolipenda Kanisa lake? Kama wewe ni mmojawapo wa wasiofuata kielelezo cha
KRISTO katika ndoa usijisikie vibaya kwani hakuna aliye mkamilifu. Hata hivyo wajibu huu
haukwepeki kwani ni agizo la MUNGU na lazima kutii maagizo yake, kumpenda MUNGU kwa moyo
waklo wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. Na kumpenda
jirani yako kama nafsi yao. Marko 12:30-31. Hivyo, hii ni nafasi yako ya kumwonyesha mwenzi
wako upendo ambao wa muda mrefu ameukosa, upendo ambao KRISTO ameuonyesa kwa kanisa lake.
Mc,Ray
0659/375263
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni