Pongezi kwa washindi wa Tuzo ya Nobeli
Jumuiya ya kimataifa imepokea vyema ushindi wa Tuzo ya Nobeli kwa msichana Malala Yousafzai wa Pakistani na Kailish Satyarthn wa Iindia. Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amenukuliwa akisema " Hii ni siku nzuri kwa watoto duniani. Watoto ambao hivi leo hawana haki ya utoto wao, elimu, kutokiukwa utu wao, wamepata sauti zao za haki ya elimu na kupinga utumikishwaji wa ajira usiyo wa haki kupitia wawakilishi hao wawili walioshinda tuzo. Nao marais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso na wa Baraza la umoja huo Herman Van Rompuy walitoa taarifa ya pamoja wakisema " Hatuwezi kuwasahau mamilioni ya watoto duniani kote ambao wananyimwa haki yao ya kupata elimu". Na kuongeza kusema huo ni ushindwa kwa wote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni