NA HIZI
NDO SABABU ZINAZO WAFANYA WANAUME WATOKE NJE YA NDOA/NJE YA MAHUSIANO YAO.
1: Mboga Mpya: Wanaume wengi huchoka kula nyama kila siku usiku badala yake hutaka kujaribu mboga mboga nazo zinakuwaje, hii ndio sababu wanaume huwa hawajali mwanamke wanayetembea nae nje ya ndoa hata kama akiwa hana mvuto hata kidogo. 2.Sio Kama zamani: Kama mwanaume ataona mpenzi wake hayuko kama zamani kwa mfano hajijali tena, amenenepa sana siku hizi, hapendi tena mambo ya mapenzi n.k sababu kama hii hupelekea wanaume wengi kutengeneza kibanda nje. 3: Mapenzi: Kama mwanaume anaona mwanamke wake anashindwa tena kumtosheleza kimapenzi au anashindwa kujaribu mambo mapya katika mapenzi, basi mwanaume huyo hutoka nje ya ndoa kujaribu kutafuta mambo mapya katika mapenzi mapya ambayo mke wake hawezi kumfanyia. 4: Kisasi: Mwanaume wakati mwingine huamua kutoka nje ya ndoa kama njia ya kupunguza machungu ya hisia zake baada ya kugundua mke au mpenzi wake anatoka nje ya ndoa. 5.Nafasi: Kwakuwa ni mara chache sana wanaume kutamkiwa mambo ya mapenzi na wanawake, wanaume wengi huwa ni vigumu kuiachia nafasi pale mwanamke mwingine anapoonyesha mapenzi na kuwa tayari kwaajili yake. "Bahati imejileta yenyewe kwanini kuilazia damu". 6.Mabishano: Kama kwenye nyumba migogoro haiishi kila siku, wanaume wengi hutafuta nyumba ndogo pembeni ili kupata sehemu ya kujilawaza na kuondoa stress zao. 7. Mapenzi kupungua: Wakati mwingine wanaume huona mapenzi katika ndoa yamepungua na huamua kubakia kwenye ndoa kwasababu ya watoto au sababu za kiuchumi, kwa maana hiyo huamua kutafuta mapenzi zaidi nje. 8. Msamaha: Kama mwanamke atamkamata ugoni mwanaume wake mara nyingi sana na mara zote akamsamehe, basi kuna uwezekano mkubwa wa mwanaume kuendelea kutoka nje kwa kuwa atajua msamaha utakuwepo tu.
MC.RAY
WHATSAPP 0659/375263 INSTAGRAM MC.RAYMONDMUSHI FACE BOOK Raymond Mushi PAGE Rayshughuli |
Shule
![Shule](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhowosffr85R15Iy8OeXGODZp5kd2v0ncDhKEPBKYhYhAU1s6Cjj7sf6d6qCwYkz-nRr7mMc1AtErm869z7-WhD5IUWXoPH-MEepRv9S3MAMZ_7sKHSvmJEdFmwxh2vFgslpN7fTH_kULGM/s1600/Tangazo.jpg)
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache
MAHUSIANO
wa wanaume karibia wote
wanajua kwamba kutoka nje ya ndoa ni makosa lakini wengi wamekuwa wakiendelea
kuwa na vimada nje.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_t8ygCiy0KgjXkXi9CKbHrtonXXePYM10AyqMkj5U9c2dJADvWbRBxA9nck4rDgD9Xdv7Bk_KuJSYyCLv710Ya3bf4zcOpVAwbjQkEUntXOvsMueNIO-H98oWFR7oE5uMJApZep-GP0XxO4twKkPaO0PKvt1UWCRqu9qHZWQKlDWrH4Pxd1qg=s0-d)
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni