Ajali ya boti yauwa 9 Guinea, 30 hawajulikani walipo
Kiasi ya watu wa tisa wamekufa na wengine 30 kutojulikana walipo kutokana na ajali ya boti iliyotokea kwenye mto Guinea. Kwa mujibu wa taarifa ya wakazi na polisi katika eneo hilo, ajali hiyo imetokea jana alasiri karibu na mji wa Contaah, wilaya ya Forecariah, iliyopo umbali wa kilometa 100 kusini/mashariki mwa Conakry. Mkazi wa Forecariah alililithibitishia shirika la habari la Uingereza Reuters kutokea kwa mkasa huo. Matukio ya ajali za boti katika eneo la Afrika Magharibi yamekuwa kama ya kawaida kutokana na kutotimizwa taratibu za usafiri salama na hasa katika maeneo ya karibu na Forecariah ambako kumekuwa na vijiji kadhaa vilivyo karibu na visiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni