Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache
Msanii wa Kenya, Atemi na mwanamuziki wa Tanzania Lady Jaydee wametoa kibao kipya kwa jina 'MOYO'.
'Moyo' ni wimbo kuhusu mapenzi ya matukio tofauti .
Katika wimbo huu Atemi anasema kuwa haijalishi penzi lina mvuto wa kiasi gani mwishowe bado linasalia kuwa penzi.
Wimbo huo uliotungwa na Atemi Oyungu ni 'single' ya kwanza kutoka album yake mpya ya tatu.
Wimbo huo umeandaliwa na R-kay ambaye pia aliandaa wimbo mwengine wa Atemi 'Usijali' akiimba na Delvin Savara wa Sauti Sol.
CHANZO BBC.
Ripoti kutoka Yemen zinasema kuwa
waasi wa Houthi wameondoka nyumba ya rais waliokuwa wameiteka katika mji
muhimu wa kusini wa bandari ya Aden baada ya mshambulizi ya ndege za
taifa la saudia kulenga eneo hilo.
Wapiganaji walio watiifu kwa
rais Abd Rabbuh Mansur Hadi wanasema kuwa wamepokea zana za kijeshi
zilizoangushwa kutoka ndege za kijeshi za saudia wakati ambapo mapigano
yanaendelea katika mji huo.
China imewaondoa zaidi ya raia wa kigeni 200 kutoka bandari hiyo.
Makumi ya raia yameripotiwa kuuawa siku chache zilizopita katika mapigano ya Aden.
CHANZO BBC
Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema
nchi yake itatekeleza wajibu wake kikamilifu kuhusiana na muafaka
uliofikiwa kuhusiana na mpango wake wa kupata nguvu za nyuklia mradi tu
wahusika wengine kwenye makubaliano hayo watekeleze wanayopasa
kuyafanya.
Akihutubia taifa hilo kupitia runinga ya nchi hiyo,
rais Rouhani ameongeza kusema mataifa 6 makuu duniani yaliyoshiriki
katika majadiliano hayo walikubali kuwa Iran ina haki ya kuendelea na
mpango huo ndani ya mipaka yake na bila kuhatarisha usalama wa mataifa
mengine.
Chini ya makubaliano hayo Iran imekubali kupunguza kiwango cha mradi huo kwa zaidi ya theluthi mbili.
CHANZO BBC.
Hivi umeshawahi kujiuliza kwamba
wafanyabiashara ya ngono ni watu wa namna gani? Ama biashara hiyo ni
biashara kama biashara zingine kivipi? Nchini Australia,maelfu ya
wafanyabiashara ya ngono bila soni wameweka bayana namna wanavyotumia
mitandao ya kijamii na kuueleza ulimwengu jinsi wanavyo fanikisha
biashara hiyo.
Huwa hawachagui wateja,Mwanafunzi mwenzangu?
Mwanasheria nimtakaye,mwanaharakati,binti yangu?dada yangu, mfanya
biashara mwenzangu wa ngono? Familia yangu! Sihitaji msaada wao.
Huo
ni baadhi ya maelfu ya ujumbe kutoka nchini Australia kwa wafanya
biashara ya ngono wanaojieleza huku wakitumia ukurasa wa
#facesofprostitution hashtag.Fukuto hili lilianza tangu mwishoni mwa
juma lililopita katika Instagram na mfanya biashara wa ngono mwenye umri
wa miaka 21 ambaye ni mhitimu wa masuala ya Historia anayejulikana kama
Tilly Lawless.
Aliamua kuzungumzia blog moja iliyoamua kurudia
kuweka kwenye ukurasa wake taarifa iliyorushwa wiki iliyopita katika
ukurasa wa gazeti maarufu lenye kuandika habari za akina mama liitwalo,
Mamamia.Blog hiyo iliandika katika maadhimisho ya miaka ishirini na
mitano mkutano wa wafanya biashara ya ngono na filamu yao ya
‘prince-charming Pretty Woman' na kudai kuwa shuhguli nzima ya biashara
ya ngono haina mvuto kama ilivyo katika filamu hiyo.
Tilly Lawless
alichukizwa na namna taarifa hiyo ilivyoweka mambo kirahisi rahisi na
kuijumuisha biashara ya ngono na kuiona biashara hiyo kama yenye madhara
.bibi huyo anashuhudia kuwa ameifanya biashara hiyo ya ngono kwa miaka
miwili lakini amejulikana hadharani miezi miwili iliyopita mjini
Sydney,mahali ambako biashara ya ngono ruksa kuifanya kisheria . na
alichukua maamuzi ya kuweka picha yake bayana katika ukurasa wake wa
Instagram kuonesha uzuri na upande wa pili wa biashara ya ngono ,sura ya
mwanamke mrembo,ambaye anajitambua na aliyechagua kuwa mfanyabiashara
ya ngono kwa mantiki ya kukipinga kilichoandikwa katika jarida la
Mamamia na blog pia.
CHANZO BBC.
Familia za wanafunzi waliouawa
katika chuo kikuu kazkazini mashariki mwa Kenya zimeenda katika eneo la
mkasa ili kuitambua miili ya waliouawa.
Zaidi ya watu 140 waliuawa
katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa Al shabaab mjini
Garissa siku ya alhamisi ambapo wapiganaji hao waliwatenganisha
wanafunzi hao kwa misingi ya kidini kabla ya kuwaua wanafunzi wa
kikristo.
Wakati huohuo mamlaka nchini Kenya imetoa mabasi ili
kuwasafirisha wanafunzi walionusurika hadi makwao,huku miili ya
waliofariki ikisafirishwa hadi mjini Nairobi.
Rais wa Somali
Hassan Sheikh Mohamoud,amesema kuwa Somalia na Kenya lazima ziimarishe
ushirikiano wao dhidi ya Ugaidi baada ya shambulizi hilo.
CHANZO BBC.
Aliyekuwa makamu wa rais nchini Zimbabwe Joice Mujuru amefukuzwa katika chama tawala ZANU-PF.
Chama
hicho kinasema alipanga njama za kumuondoa mamlakani rais Robert Mugabe
mbali na kukiharibia jina chama hicho- madai ambayo ameyakana hapo
mbeleni .
Bi Mujuru alipigana vita vya Guerilla pamoja na Mugabe
miaka ya sabini dhidi ya uongozi wa weupe na alionekana kama mrithi
wake,kabla ya kukosana naye mwaka uliopita swala lililomfanya kufutwa
kazi kama makamu wa rais mnamo mwezi Disemba.
Waandishi wanasema alishtumiwa sana na mke wa Mugabe, Grace ambaye anaongoza wanawake katika chama hicho.
CHANZO BBC.
Kim akimpa taarifa mumewe Kanye West juu ya tatizo linalomkabili.
Mwanamama nguli na nyota wa kipindi
cha runinga cha The Keeping Up with the Kardashians,Kim West ambaye ana
mtoto mwenye umri wa miezi 21 North West aliyezaa na mumewe Kanye
West,imeelezwa na mumewe huyo Kanye ,mkewe hataki chochote katika
ulimwengu huu zaidi ya kupata mtoto mwingine ,lakini madaktari
wamemuonya anaweza kukabiliwa na hatari kiafya.
Katika kipande cha
kipindi kinachofuata cha kipindi cha mwanamama huyo ambacho kitarushwa
katika runinga ya E’ inayojihusisha na masuala ya burudani na huenda
kipande hicho kitarushwa mwishoni mwa wiki hii ,kipande hicho
kinamuonesha Kim akielezea alichoambiwa na daktari wake kuwa anajaribu
kumficha Kanye West anachotakiwa kwenda kufanyiwa na madaktari kuondoa
kitu kilichoko kwenye kizazi chake.
Na ilipobidi kumkabili mumewe
huyo, ambaye ni nguli wa muziki wa tambo,alipomwambia juu ya suala hilo
tete, alikubaliana nalo na kumwambia endapo atafanikiwa kupata mtoto wa
pili atakuwa wa mwisho kwasababu kondo la uzazi linakua kwenye kizazi
chake. Mke wa Kanye West
lakini baadaye mrembo huyo
alionekana kukata tamaa ya kupata mtoto mwingine,na akaeleza wazi kuwa
alipokuwa mjamzito wa mtoto wao wa sasa North,alikuwa akiwaambia watu
wake wa karibu kwamba hakuna kiwango cha pesa duniani atakachoweza
kulipwa kurejea tena katika maumivu ya uchungu wa kuzaa.
Lakini,kwasasa
hakuna kitu ninachokihitaji zaidi ulimwenguni kama kuwa mjamzito
tena,nina pata hasira kidogo kwamba watoto wangu wataachana miaka
kadhaa.
Siku za karibuni Kim alitoa ya moyoni kwa kueleza kwamba
ulikuwa ni muujiza kuipata mimba ya mtoto wake North kwasababu madaktari
walisha mwambia kuwa milele hataweza kubeba ujauzito .
chanzo bbc.
Machoni anatazamika, lakini moyoni alikuwa hana raha.
Mwanamke mmoja nchini India amekuwa
na mazoe na tabia kujengeka ya kukojolea vikombe vya wakweze kila
iitwapo leo kwa muda wa mwaka mmoja ,zake zilitimia baada ya kufumwa na
mama mkwe wake jikoni akiwa amekinga buli la chai anakojoa ndaniye.
Chanzo
kisa na sababu ya kadhia hiyo kutokea ni wakweze kumpiga marufuku mtoto
wao wa kiume kufanya kazi za nyumbani na ndipo mkwe huyo alipoamua
kujilipiza kisasi kwa kukojolea vikombe vya wakweze kwa zaidi ya mwaka
mmoja.Rekha Nagvanshi, mwenye umri wa miaka 30,alikuwa akiishi nyumba
moja yeye na mumewe Deepak,mwenye miaka 34, katika wilaya ya Indore
jimbo la Madhya Pradesh,pamoja na wakweze .
Mwanamke huyo alidai
kwamba ingekuwa bora angeishi na nduguze kuliko kuishi kwa wakeze,na
alisema kwamba hakuwa na furaha namna ndoa yake ilivyoendeshwa na
alikuwa akijihisi anatendewa visivyo na hapati matunzo muafaka.Rafiki wa
mwanamke huyo , Alia Kohli, mwenye umri wa miaka 32, alisema kwamba
rafikiye hakuwa na furaha na ndoa yake tangu siku ya kwanza ya harusi na
mumewe alikuwa akimtenda kama mtumwa na mwanamke huyo ameamua kuwa
imetosha.
Lakini chakushangaza baada ya kuondoka kuelekea kwa
wazazi wake , mara aliomba kurejea ukweni ati tu kwasababu ya majaaliwa
ya mtoto wao wa kike aliye na umri wa miaka minne ili aendelee kumpa
malezi yake,na alipo rejea kwa wakweze aliweka masharti ya mumewe
kumpikia chakula,kumkandakanda miguu yake na kumfulia nguo zake zote
lakini wazazi wa kijana huyo hawakuridhishwa na masharti hayo ,hivyo
waliweka mpango wa kukomesha masharti hayo. Tabasamu usoni rohoni anakereketwa
Mume wa mwanamke huyo Deepak
anasema kwamba yeye alikuwa radhi na masharti ya mkewe lakini wazazi
wake walimjia juu na kumsema kwamba hiyo haikubaliki kwani anamshurtisha
mtoto wao kama mtumwa.
hata hivyo inaelezwa kwamba,wazazi wa
mwanaume huyo walikuwa na kawaida ya kuwatembelea watoto wao mara moja
kwa wiki, kitendo kilichokuwa kikimkera mno mkamwana wao na akaamua
kuwatenda, wazazi walipogundua hila yake walisema kwamba walijua mkwe
wao hawapendi lakini hawakufikiria kwamba anaweza kuwatenda namna
hiyo,maana alikuwa akitabasamu na kuwapa chai nao waliipokea,lakini siku
moja mamake Deepak niliingia ghafla jikoni na kumfuma mkwe akikojolea
birika ya chai.
wazazi hao mke Suraj na mume waliamua kwenda kutoa
taarifa polisi ,na huko wakatwambia masuala ya namna hiyo
hawashughuliki nayo,wazazi wa mwanaume huyo wakadai sheria ichukue
mkondo wake maana si jambo rahisi kwa mwaka mmoja mtu akojolee birika
yenye chai na aachiliwe hivi hivi, wanataka haki itendeke.
Kufuatia
kisanga hicho imejulikana familia iko mbioni kulipeleka mahakamani
suala hilo na kwamba Rekha na mumewe Deepak wametengana.
CHANZO BBC.
Maandamano Garissa
Wananchi wa mji wa Garissa nchini
Kenya wamefanya maandamano kupinga vitendo vya kundi la Al Shabaab,
lililoshambulia chuo kimoja kikuu mjini humo na kuwaua watu 147 wengi
wao wakiwa wanafunzi hapo jana.
Waandamanaji pia wameelezea
kutoridhika na vyombo vya usalama nchini humo wakisema havikuchukua
hatua za kutosha kutoa ulinzi kwa waliouawa na kwa raia wengine kwa
jumla.
Wazazi, jamaa na marafiki wa wanafunzi waliouawa katika
chuo kikuu cha Garissa wamekuwa wakiendelea kuwasili katika eneo hilo
kuitambua miili ya wapendwa wao.
Waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu . Garissa
Serikali ya Kenya imekuwa
ikiwasafirisha manusura wa shambulio hilo kwa mabasi kuelekea makwao
huku miili ya waliouawa ikisafirishwa mjini Nairobi.
Wakati huo
huo rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamoud, amesema Somalia na Kenya
zinafaa kuimarisha uhusiano wao katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Tamko hilo linajiri siku moja baada ya shambulio hilo la Alshaabab katika chuo kimoja kikuu mjini Garrisa.
chanzo bbc.
Wanachama Saba (7) wa klabu ya Simba ya Dar es salaam kutoka tawi la
Mpira na Maendeleo (maarufu kama Simba UKAWA) ambalo limewahi
kutangazwa kufutwa wamefariki dunia katika ajali ya basi mkoani
Morogoro.
Wanachama hao wakiwa katika basi lao walikuwa
wakielekea Shinyanga kwa ajili ya kuipa nguvu Simba ambayo inatarajiwa
kushuka katika dimba la CCM Kambarage kuikabili Kagera Sugar katika
mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kesho..
Vifo hivyo vimefikia 7 baada ya watano kufa palepale na wengine wawili
waliokuwa majeruhi kufariki katika hospitali ya mkoa wa Mororgoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Leonard Paul amethibitisha
habari hizi na kusema kuwa majeruhi wamebaki 13 na kufanya vifo kufikia
saba hadi majira ya saa 2 usiku wa April 03.
sherehe za hadhara.
Kijiji kimoja nchini India kilichoko
pwani ya Goa kimeweka sheria ya kuzuia wanandoa ama wapenzi kubusiana
hadharani ,kwa madai kuwa wenyeji wa maeneo hayo hawapendi tabia za
kimagharibi kwenye eneo lao.
Bunge la kijiji hicho liitwalo
Salvador-de-Mundo,ambalo liko kilomita nane Kaskazini ya mji wa Goa
kwenye mji wa Panaji, azimio hili limepitishwa mapema wiki hii
likiwaonywa wenye kufanya sherehe za hadhara wasijisahaulishe sheria
hiyo na kuoneshana mahaba hadharani.
Tumeamua kulipitisha azimio
hili baada ya kupokea malalmiko kutoka kwa wanakijiji juu ya watu
wanaobusiana hadharani.hii ndio njia pekee ya kulimaliza suala hili
anasema chifu msaidizi wa kijiji hicho Reena Fernandes .
Bibi huyo
ambaye ni chifu msaidizi ameongeza kwamba malalamiko yao waliyapeleka
kwa viongozi wa kijamii lakini hawakupata mrejesho wala hatua zozote
kuchukuliwa na hivyo wakaamua kuchukua sheria mikononi na kupasisha
azimio la marufuku ya kunywa pombe hadharani na kupiga muziki hadharani
kwa sauti kubwa.
Hata hivyo ,amekataa kuzungumzia chochote juu ya hatua za adhabu zitakazo chukuliwa kwa wataovunja sheria hiyo .
Mwanakijiji
mmoja Savio Rebeiro amesema kwamba tumezizuia pwani zinazovutia
utalii,maana mara kwa mara huwa tunashuhudia wapenzi wawili wafanyao
matendo yanayo tukera . rahaje???????
Ukanda huo wa bahari ya hindi
wenye biashara kubwa ya uvuvi kwa sasa wamesambaza mabango yenye ujumbe
wa elimu juu ya katazo hilo.
Pwani za Goa zimejaa mchanga zenye mvuto wa kipekee kwa mamilioni ya watalii kutoka Magharibi na katazo hilo limetia doa utalii.
Naye
waziri mkuu Narendra Modi mwenye asili ya Kihindu wa chama cha
Bharatiya Janata wiki hii aliweka marufuku ya wanawake waajiriwa kuvaa
suruali za jinzi na singilendi katika ofisi za serikali.
Mwaka
uliopita waziri wa Goa alitaka itungwe sheria ama amri ya katazo la
uvaaji bikini katika pwani zote na alipokea upinzani mkubwa kutoka kwa
jamiina tasnia ya utalii.
CHANZO BBC.
Zaidi ya wapiganaji wa kigeni elfu
ishirini na watano kutoka mataifa mia moja walisafiri kwa nia na malengo
ya kujiunga na makundi ya kijeshi kama al-Qaeda na Islamic State (IS),
taarifa ya umoja wa mataifa imeeleza hayo.
Taarifa hiyo imeeleza
pia kwamba wapiganaji wageni ulimwenguni idadi yao imeongezeka mpaka
kufikia asilimia sabini na moja katikati ya mwaka 2014 na march mwaka
huu.
Nchi za Syria na Iraq ndizo nchi zinazolengwa kwa ukaribu
zaidi na ndicho kitovu cha vijana wanaomaliza mazomo yao na kugeuka kuwa
wenye msimamo mkali wa kidini.
Na pia taarifa hiyo imebainisha
kuwa endapo kundi la IS lingeshindwa nchini Syria na Iraq,sasa
wapiganaji hao kutoka nchi za kigeni wamesambaa ulimwenguni .
Nalo
baraza la usalama la umoja wa mataifa liliwaomba wataalamu wa masula ya
kijeshi miezi sita iliyopita kuchunguza vitisho vya askari wa kigeni
wanaojiunga na kundi la Is na makundi mengine ya kigaidi.
Katika
ripoti iliyowasilishwa kwenye baraza hilo mwishoni mwa mwezi uliopita
,na wataalamu wakaeleza kuwa ongezeko la wapiganaji wa nchi za kigeni
zinazidi kuongezeka kulinganisha na muongo mmoja uliopita .
Maelfu
ya wapiganaji wa kigeni ambao hufanya safari hadi nchini Syria ,Falme
za Kiarabu na Iraq huko hufanya makao na kufanya kazi na kumalizia
masomo ya elimu ya juu kwa wenye msimamo mkali kamalivyowahi kutokea
kwatika nchi ya Afghanistan miaka ya 1990 .
Syria na Iraq
inasemekana ina makaazi elfu ishirini na mbili kwa wapiganaji hao wa
kigeni ,pia nchini Afghanistan makaazi elfu sita na mia tano na maelfu
ya makaazi nchini Yemen, Libya, Pakistan na Somalia.
CHANZO BBC.
Kadinali Raymond Burke mwenye asili
ya Marekani ameenguliwa na Papa Francis katika wadhifa wake wa
mwenyekiti wa bodi katika kanisa katoliki,ametoa onyo kwamba kuna
viashiria vya kanisa hilo kuupigia chapuo ushoga, kauli hii Burke
aliiotoa wakati alipokuwa akihojiwa na tovuti moja ya Italy ya La Nuova
Bussola Quotidiana mara baada tu ya kuenguliwa kwenye wadhifa wake.
Mwandishi
wa BBC anasema hii ni ishara nyingine ya jinsi viongozi wa dini
waandamizi wanavyochukulia hatua juu ya masuala kama vile ushoga na
talaka , wakati wengine wanatakiwa kuyachukulia mambo kwa utuvu na
uangalifu wa hali ya juu.
chanzo bbc.
Idhaa yako ya kiswahili ya BBC imekuandalia ukurasa wa habari za moja kwa moja kufuatia shambulizi la chuo kikuu nchini Kenya.
14.00pm:Kwa ufupi wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa
Takriban watu 15 wanaodaiwa kufinika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.
Watu
hao wanaodaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi
wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.
Hatahivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja unusu.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho waliosalimika
Mwandishi wa BBC mjini humo
anasema kuwa walinzi wawili waliuawa katika lango la chuo hicho huku
maafisa wawili wa polisi waliokuwa wakilinda chuo hicho pamoja na
wanafunzi wakijeruhiwa.
Walioshuhudia wanasema kuwa kumekuwa na majeruhi mengi ndani ya chuo hicho.
Mwandishi wetu anasema kuwa wapiganaji hao bado wako ndani ya chuo hicho na wamewateka nyara watu kadhaa. Wanafunzi waliotoroka shambulizi mjini Garissa Kenya
Jeshi la Kenya KDF ,maafisa wa
polisi na amabulansi wamefika katika eneo la tukio na sasa wameingia
ndani ya majengo ya chuo hicho ambapo kumekuwa na ufyatulianaji wa
risasi kati ya washambuliaji na maafisa wa jeshi.
13.40pm:Waislamu
na wakristo waliotekwa ndani ya Jumba hilo la Chuo kikuu cha garissa
wamedaiwa kutawanywa kabla ya waislamu 15 kuwachiliwa huru kulingana
na msemaji wa kundi hilo la Alshabaab.
13.35pm:Serikali ya kenya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulihutubia taifa kufuatia shambulizi hilo la chuo kikuu cha Garrisa mapema leo.
13.30pm:Alshabaab: Maafisa wa Polisi wa kenya
kundi la wapiganaji wa Alshabaab limesema kuwa liko ndani ya Chuo hicho kikuu na limewatawanya waislamu na wakristo
13.20pm:Wapiganaji
wamedaiwa kuwateka nyara wanafunzi na kuwaua watu 14 katika chuo hicho
kulingana na wafanyikazi wa msaada na maafisa wa polisi.Takriban watu 65
wengine wamejeruhiwa baada ya washambuliaji kuvamia chuo hicho.Vituo
vya habari nchini kenya hatahivyo vinaiweka idadi hiyo kuwa watu 16.
13.05pm:Idadi ya watu waliouawa kufuatia shambulizi la wapiganaji wa kundi la alshabaab imefikia 14
13.03pm:Al shabaab
Alshabaab lakiri kutekeleza shambulizi
Kundi la wapiganaji wa Al-shabaab limekiri kutekeleza shambulizi
katika chuo kikuu cha Garissa Kaskazini mashariki mwa Kenya huku
likiwaua watu 14
12.47pm:Wanafunzi wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya
Chuo hicho cha Garissa kina takriban wanafunzi 1000, na wafanyikazi wengine.
12.30pm Wanafunzi:
Wanafunzi waliodaiwa kutoroka
Baadhi ya wanafunzi wamedaiwa kutoroka kutoka mabweni waliokuwa wakilala
12.20pm:Wapiganaji Wapiganaji
Wapiganaji hao wanaodaiwa kuwa watano wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo la Chuo kikuu .
12.18pm:Kenya Red Cross Maafisa wa polisi wakikabiliana na wapiganaji huko Garissa kenya
Shirika la msalaba mwekundu
nchini Kenya linasema kuwa watu 30 wamejeruhiwa huku wanne kati yao
wakiwa na majeraha mabaya..Kwa sasa shirika hilo linawasafirisha
madaktari katika eneo hilo. 11.30am Idadi ya watu
waliouawa kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini
mashariki mwa Kenya imefikia watu sita huku wengine 29 wakidaiwa
kujeruhiwa. CHANZO BBC.
Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imesema kuwa kura ya maoni ya katiba
inayopendekezwa, haitaweza kufanyika tena tarehe 30 April hadi hapo
itakapotangazwa tarehe nyingine tena.
NEC imesema sababu ya
kuhairisha kura hiyo April 30 ni kutokana na kutokamilika kwa zoezi la
uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura.
Unakumbuka zamani Wabunge wa upinzani walikuwa wakiona hawatendewi haki
na Spika wanasusa na kuondoka Bungeni, kwahiyo mambo mengi yanajadiliwa
bila wao kuwepo. Ila kwa sasa wanambinu tofauti ambayo wakiona
hawatendewi haki wanasimama juu na kuanza kugonga gonga meza na kupiga
kelele hadi Bunge linaharishwa
Msala uliompata Mchungaji Gwajima wa kumtolea maneno yenye kuudhi
Askofu wa Kanisa Katoliki Mwadhama Polycap Kadinali Pendo na kisha
kuhojiwa polisi na kupata mshtuko, kuzimia hadi kulazwa, Mume wa Flora
Mbasha, anasema hayo ni malipo ya Mungu kwake kutokana na kilio chake
baada ya Mchungaji huyo kusambaratisha ndoa yake .
“Ile hali ya
Gwajima ni malipo. Mimi nilishasema jamani, mtu akikutendea ubaya malipo
ni hapahapa duniani, hakuna kwingine. Mimi ndoa yangu haipo, mke wangu
anajua yeye anavyoishi. Kwa hivyo mimi nimekuwa nikiishi kwa
manung’uniko kila siku, unadhani nini kitatokea kwake?” amefunguka
Emmanuel Mbasha
Meli ya uvuvi ya Urusi iliyozama kwa dakika kumi na tano tu
Boti ya uvuvi ya Urusi imezama
katika visiwa vya Kamchatka , ikiwa na mabaharia wapatao hamsini na
wanne ambao inadhaniwa kuwa wamekufa maji wote.
Watu wapatao
sitini na watatu wameopolewa ambao nao walikuwa ndani ya boti hiyo ya
uvuvi,wengine wamekumbwa na homa ya mapafu na wengine kumi na watano
wameripotiwa kuwa hawaonekani.
Taarifa za awali zinasema kwamba
kabla meli hiyo ya uvuvi haijazama ilikuwa na watu wapatao miamoja na
thelathini na mbili ,uchambuzi unaeleza kuwa sabini na nane kati yao ni
raia wa Urusi na arobaini na wawili ni raia wa Myanmar. Wengi wao
walikuwa wanatokea maeneo ya Vanuatu, Latvia na Ukraine na nahodha ni
miongoni mwa waliopoteza maisha.
Kikosi cha uopoaji kinaendelea na kazi ya oukozi ambapo mpaka sasa wanatafuta abiria hao waliopotea wapatao kumi na watano .
Nahodha
wa kikosi cha uongozi ambaye ni miongoni mwa mabaharia wa kikosi cha
uopoaji ishirini na sita anasema kwamba pengine chanzo cha ajali hiyo ni
hali mbaya ya hewa, na wakati meli hiyo ilipokuwa ikizama ,kulikuwa na
barafu,upepo mkali, mawimbi yenye urefu wa futi kumi. Na maji ya bahari
yalikuwa karibu yanaganda kwa nyuzi joto 32 .
Inaelezwa kwamba
manusura wa ajali hiyo walikuwa wanauwezo wa kudumu katika maji hayo kwa
dakika ishirini tu,ingawa mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo ni cha
kukisia tu.
Maji yalifurika kwenye chumba cha ingini ya meli hiyo
na kuanza kuzama ndani ya dakika kumi na tano kimesema kitengo cha
dharula cha Urusi,na kusema kwamba pengine meli hiyo iligonga eneo la
karibu na chumba cha ingini na kuwa sababu ya ajali hiyo.
Sergei
Khabarov amesmea kwamba kiwango cha abiria na mizingo katika meli za
wavuvi lazima kizingatiwe na kisizidi uwezo wa vyombo hivyo.
chanzo bbc.
Wapiganaji waliofunika nyuso zao
wameshambulia eneo la chuo kikuu cha Garissa kaskazini mwa Kenya karibu
na mpaka wa taifa hilo na Somalia.Milio mikali ya risasi pamoja na
milipuko imesikika katika chuo kikuu cha Garissa mjini humo.
Maafisa wa usalama wa Kenya wamethibitisha kuwa watu wawili wamefariki huku wanne wakijeruhiwa.
Wakaazi wa eneo hilo wametakiwa kukaa mbali na eneo la chuo hicho.
Haijulikani
ni nani aliyekusika na shambulizi hilo ,lakini kundi la wapiganaji wa
Somalia Al shabaab limetekeleza misururu ya mashambulizi mjini Garissa
pamoja na maeneo mengine ya Kenya tangu mwaka 2011 wakati wanajeshi wa
kenya walipopelekwa Somalia.
CHANZO BBC.
Binti aliyejulikana kwa jina la Mariam Moshi (23), mkazi wa Mwananyamala
Ujiji, aliponea chupuchupu kuuawa na wagonjwa wenye hasira kali
waliolazwa katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kudaiwa kuiba nguo
za wagonjwa. Mariam anadaiwa kuiba Kitenge kipya na taulo. Mwenyewe
alipoulizwa alisema Kitenge tu ndio amekiiba hospitalini hapo ila taulo
alilokuwa amejifunga ndani ya dera alilovaa, alisema aliliiba katika
gesti aliyokuwa amelala siku hiyo.. Aliomba msamaha kwa kitendo
alichokifanya, akisema kinatokana na maisha magumu
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Polisi
Mkoa wa Pwani linaendesha oparesheni kali ya aina yake ya kuwasaka watu
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliowavamia, kuwauwa askari wawili na
kumjeruhi mmoja na kisha kupora bunduki aina ya SMG. Tukio hilo
limetokea tarehe 30/03/2015 majira ya saa mbili usiku huko barabara ya
Kilwa Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Katika tukio
hilo majambazi wapatao 8 hadi 10 wakiwa
na mapanga na silaha zingine waliwavamia ghafla askari watatu waliokuwa
kazini katika eneo la kizuizi cha Polisi kilichopo kijiji cha Kipara
mpakani Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Majambazi hao
wakiwashambulia ghafla askari hao kisha kupora silaha aina ya SMG ikiwa
na risasi 30 ndani ya magazine na kutokomea kusikojulikana. Majina ya askari wa Wilala ya Kipolisi ya Mbagala waliouawa ni kama ifuatavyo: D.2865 SGT FRANCIS, E.177 CPL MICHAEL, CHANZO 5EATV.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kuwa serikali imeiagiza Tume ya
Taifa ya Uchaguzi kutoa ratiba kamili kuhusu zoezi la uandikishwaji
Wapiga Kura kwa BVR pamoja na hatma ya Kura ya Maoni ya Katiba Mpya.
Pinda ameyasema hayo wakati akiahirisha Bunge majira ya saa 6 usiku wa
kuamkia Alhamis tarehe 02 April, 2015 ambapo amedai kuwa tayari serikali
imekwisha lipia pesa zote kwa ajili ya mashine zote za kuandikishia (BVR).
“Serikali imekwishatoa pesa kwa ajili ya mashine zote za BVR
kilichobaki ni kwa Tume kupanga ratiba yao, tuna imani kuwa mashine zote
zikifanya kazi zoezi la uandikishwaji wapiga kura litamalizika kwa
wakati” Amesema Pinda
Amesema ameongea na Mwenyekiti wa tume hiyo leo (April 01) na imemuhakikishia kuwa itatangaza ratiba nzima kabla ya Pasaka.
Kuhusu ugawaji wa Katiba Pendekezwa amesema kuwa tayari nakala
1,141,300 kwa upande wa Tanzania Bara na nakala 210,000 kwa upande wa
Zanzibar zimekwisha sambazwa.
Kuhusu muswada wa mahakama ya
Kadhi, Pinda amesema serikali imefurahishwa na uamuzi wa muswada huo
kuondolewa kwa kuwa itapata muda wa kutosha kujadiliana na wadau na
kutoa elimu zaidi kuhusu umuhimu wa Mahakama hiyo.
Bunge
limeahirishwa hadi tarehe 12 Mei, 2015 kwa ajili ya mkutano wa 20 likiwa
limejadili na kupitisha miswada 14 kati ya 21 iliyokuwa imepangwa
katika mkutano huu uliomalizika leo.
Kabla ya kuahirishwa, bunge
limefanya maamuzi ya kupitisha muswada wa uhalifu wa kimitandao huku
likiwa na wabunge wasiofikia nusu ya wabunge wote kama inavyotakiwa kwa
mujibu wa kanuni.
Youssou Ndour ndiye mwanamuziki tajiri barani Afrika
Usanii wa muziki ni miongoni mwa kazi zinazolipa vizuri duniani.
Hatahivyo si kila mtu anayefanikiwa katika sekta ya muziki.
Kulingana na mtandao wa capital Fm nchini Kenya,kwa wewe kufanikiwa ni sharti uipende sekta hii pamoja na uwajue wateja wako.
Hivyo ndivyo wasanii wengi wa muziki wameweza kujitengezea jina duniani.
Na
je, unawajua wanamuziki tajiri barani Afrika?Orodha ya wanamuziki 10
walio matajiri barani afrika kulingana na Answers Afrika itakushangaza.
Hii Hapa.
01.Youssou N'Dour - Senegal.
02.P-Square- Nigeria
03.D'banj - Nigerian
04.Koffi Olomide - DRC
05.Salif Keita - Mali
06.Fally Ipupa DRC
07.Face Idibia - Nigeria
08.Hugh Masekela - South Africa
09.Banky W - Nigeria
10.Jose Chameleon - Uganda
Mtu aliyekuwa na umri mkubwa duniani kutoka nchini Japan amefariki wiki kadhaa baada ya kusherehekea miaka 117 tangu azaliwe.
Misao Okawa alifariki katika kituo cha uangalizi mjini Osaka,mji ambao alizaliwa mwaka wa 1898.
Okawa amewaacha vitukuu sita na wajukuu wanne .
Kufuatia kifo chake kuna madai kwamba kumesalia watu wanne pekee wanaodaiwa kuwa hai ambao walizaliwa karne ya kumi na tisa.
Wote ni Wanaume huku mwanamume wa mwisho akifariki mwaka 2013.
CHANZO BBC.
Raia wa Yemen wakikatika Ghuba ya Aden kwa boti ndogo
Mashirika ya umoja wa mataifa yamesema kuwa mamia ya raia wa Yemen
wamevuka ghuba ya Aden kwa kutumia boti ndogo na kuingia nchini Somalia,
Djibouti na Somaliland wakikimbia mapigano nchini mwao. Shirika la
umoja wa mataifa la UNHCR limesema kuwa linaangalia eneo zuri kwaajili
ya kuweka kambi ya wakimbizi kwaajili ya raia hao. Wakati huo huo
wakimbizi kutoka nchini Somalia bado wanaendelea kuingia nchini Yemen
kuepuka njaa na machafuko nchini mwao. Shirika hilo la UNHCR linasema
kuwa Yemen inawahifadhi wakimbizi wapatao 238,000 kutoka Somalia.
Mwandishi wa BBC Africa Mary Harper anasema wazo la Yemen kufikiria kuwa
na kambi za wakimbizi nchini Somalia si la kawaida kwa kuwa ni kawaida
kwa raia nchini humo kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya mara
kwa mara hali ambayo haiwezi kuwa eneo zuri kwa wakimbizi kuhifadhiwa.
chanzo bbc.
Katika Kisiwa cha Mafia mkoa wa Pwani mama aitwaye Mwasiti Ally amekuwa
akiwafungia ndani watoto wake ndani kwa muda wa miaka 10 sasa kwa madai
kuwa ni wagonjwa wa akili. Watoto hao huko ndani ya chumba wote
wamebadilika na kuwa na afya mbaya huku kucha za mikononi na miguuni
kurefuka sana, nywele zimekua ndefu kiasi cha kutisha na sura zao
kuonekana kama za misukule na kuwa kama walemavu wa miguu. Alianza
kuugua mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza kuzaliwa, cha ajabu, kila mwaka
mwingine akafuatia hadi wa tatu. Mama huyo anadai Sababu kubwa ya
kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 anasema ni kwaajili ya usalama wao
maana anaamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.
Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini
Nigeria Muhammadu Buhari ameelezea mashambulizi yanayotekelezwa na
kundi la wapiganaji wa Boko Haram kama tatizo kuu linalokabili taifa
hilo.
Katika hotuba aliyotoa katika runinga za Nigeria,kiongozi
huyo wa kijeshi zamani amesema kuwa serikali yake itafanya kila juhudi
kuangamiza ugaidi.
Vilevile amesema kuwa atakabiliana na jinamizi la ufisadi.
Bwana Buhari ambaye anachukua wadhfa wa urais kuanzia mwezi ujao,alimsifu mpinzani wake na rais anayeondoka Goodluck Jonathan.
Alimtaja kuwa kiongozi anayehitaji heshima.
CHANZO BBC.