![](https://scontent-ams.xx.fbcdn.net/hphotos-xpt1/v/t1.0-9/s480x480/11091283_1186208884726861_7022082636018690274_n.jpg?oh=d62d5a4db06c92e9d52bd698cff8c845&oe=55AA412A)
Binti aliyejulikana kwa jina la Mariam Moshi (23), mkazi wa Mwananyamala Ujiji, aliponea chupuchupu kuuawa na wagonjwa wenye hasira kali waliolazwa katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kudaiwa kuiba nguo za wagonjwa. Mariam anadaiwa kuiba Kitenge kipya na taulo. Mwenyewe alipoulizwa alisema Kitenge tu ndio amekiiba hospitalini hapo ila taulo alilokuwa amejifunga ndani ya dera alilovaa, alisema aliliiba katika gesti aliyokuwa amelala siku hiyo.. Aliomba msamaha kwa kitendo alichokifanya, akisema kinatokana na maisha magumu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni