Garissa Kenya
Wapiganaji waliofunika nyuso zao
wameshambulia eneo la chuo kikuu cha Garissa kaskazini mwa Kenya karibu
na mpaka wa taifa hilo na Somalia.Milio mikali ya risasi pamoja na
milipuko imesikika katika chuo kikuu cha Garissa mjini humo.
Maafisa wa usalama wa Kenya wamethibitisha kuwa watu wawili wamefariki huku wanne wakijeruhiwa.Wakaazi wa eneo hilo wametakiwa kukaa mbali na eneo la chuo hicho.
Haijulikani ni nani aliyekusika na shambulizi hilo ,lakini kundi la wapiganaji wa Somalia Al shabaab limetekeleza misururu ya mashambulizi mjini Garissa pamoja na maeneo mengine ya Kenya tangu mwaka 2011 wakati wanajeshi wa kenya walipopelekwa Somalia.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni