Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 1 Aprili 2015

TAARIFA KUHUSU ASKARI KUUAWA.


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Pwani linaendesha oparesheni kali ya aina yake ya kuwasaka watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliowavamia, kuwauwa askari wawili na kumjeruhi mmoja na kisha kupora bunduki aina ya SMG.
Tukio hilo limetokea tarehe 30/03/2015 majira ya saa mbili usiku huko barabara ya Kilwa Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Katika tukio hilo majambazi wapatao 8 hadi 10 wakiwa na mapanga na silaha zingine waliwavamia ghafla askari watatu waliokuwa kazini katika eneo la kizuizi cha Polisi kilichopo kijiji cha Kipara mpakani Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Majambazi hao wakiwashambulia ghafla askari hao kisha kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30 ndani ya magazine na kutokomea kusikojulikana.
Majina ya askari wa Wilala ya Kipolisi ya Mbagala waliouawa ni kama ifuatavyo:
D.2865 SGT FRANCIS,
E.177 CPL MICHAEL,

CHANZO 5EATV.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni