Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini
Nigeria Muhammadu Buhari ameelezea mashambulizi yanayotekelezwa na
kundi la wapiganaji wa Boko Haram kama tatizo kuu linalokabili taifa
hilo.
Katika hotuba aliyotoa katika runinga za Nigeria,kiongozi
huyo wa kijeshi zamani amesema kuwa serikali yake itafanya kila juhudi
kuangamiza ugaidi.Vilevile amesema kuwa atakabiliana na jinamizi la ufisadi.
Bwana Buhari ambaye anachukua wadhfa wa urais kuanzia mwezi ujao,alimsifu mpinzani wake na rais anayeondoka Goodluck Jonathan.
Alimtaja kuwa kiongozi anayehitaji heshima.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni