Kijiji kimoja nchini India kilichoko pwani ya Goa kimeweka sheria ya kuzuia wanandoa ama wapenzi kubusiana hadharani ,kwa madai kuwa wenyeji wa maeneo hayo hawapendi tabia za kimagharibi kwenye eneo lao.
Bunge la kijiji hicho liitwalo Salvador-de-Mundo,ambalo liko kilomita nane Kaskazini ya mji wa Goa kwenye mji wa Panaji, azimio hili limepitishwa mapema wiki hii likiwaonywa wenye kufanya sherehe za hadhara wasijisahaulishe sheria hiyo na kuoneshana mahaba hadharani.
Tumeamua kulipitisha azimio hili baada ya kupokea malalmiko kutoka kwa wanakijiji juu ya watu wanaobusiana hadharani.hii ndio njia pekee ya kulimaliza suala hili anasema chifu msaidizi wa kijiji hicho Reena Fernandes .
Bibi huyo ambaye ni chifu msaidizi ameongeza kwamba malalamiko yao waliyapeleka kwa viongozi wa kijamii lakini hawakupata mrejesho wala hatua zozote kuchukuliwa na hivyo wakaamua kuchukua sheria mikononi na kupasisha azimio la marufuku ya kunywa pombe hadharani na kupiga muziki hadharani kwa sauti kubwa.
Hata hivyo ,amekataa kuzungumzia chochote juu ya hatua za adhabu zitakazo chukuliwa kwa wataovunja sheria hiyo .
Mwanakijiji mmoja Savio Rebeiro amesema kwamba tumezizuia pwani zinazovutia utalii,maana mara kwa mara huwa tunashuhudia wapenzi wawili wafanyao matendo yanayo tukera .
Pwani za Goa zimejaa mchanga zenye mvuto wa kipekee kwa mamilioni ya watalii kutoka Magharibi na katazo hilo limetia doa utalii.
Naye waziri mkuu Narendra Modi mwenye asili ya Kihindu wa chama cha Bharatiya Janata wiki hii aliweka marufuku ya wanawake waajiriwa kuvaa suruali za jinzi na singilendi katika ofisi za serikali.
Mwaka uliopita waziri wa Goa alitaka itungwe sheria ama amri ya katazo la uvaaji bikini katika pwani zote na alipokea upinzani mkubwa kutoka kwa jamiina tasnia ya utalii.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni