Wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa
Familia za wanafunzi waliouawa
katika chuo kikuu kazkazini mashariki mwa Kenya zimeenda katika eneo la
mkasa ili kuitambua miili ya waliouawa.
Zaidi ya watu 140 waliuawa
katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa Al shabaab mjini
Garissa siku ya alhamisi ambapo wapiganaji hao waliwatenganisha
wanafunzi hao kwa misingi ya kidini kabla ya kuwaua wanafunzi wa
kikristo.Wakati huohuo mamlaka nchini Kenya imetoa mabasi ili kuwasafirisha wanafunzi walionusurika hadi makwao,huku miili ya waliofariki ikisafirishwa hadi mjini Nairobi.
Rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamoud,amesema kuwa Somalia na Kenya lazima ziimarishe ushirikiano wao dhidi ya Ugaidi baada ya shambulizi hilo.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni