Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 1 Aprili 2015

RAIA WA YEMEN WAKIMBILIA SOMALIA.


Raia wa Yemen wakikatika Ghuba ya Aden kwa boti ndogo
Mashirika ya umoja wa mataifa yamesema kuwa mamia ya raia wa Yemen wamevuka ghuba ya Aden kwa kutumia boti ndogo na kuingia nchini Somalia, Djibouti na Somaliland wakikimbia mapigano nchini mwao. Shirika la umoja wa mataifa la UNHCR limesema kuwa linaangalia eneo zuri kwaajili ya kuweka kambi ya wakimbizi kwaajili ya raia hao. Wakati huo huo wakimbizi kutoka nchini Somalia bado wanaendelea kuingia nchini Yemen kuepuka njaa na machafuko nchini mwao. Shirika hilo la UNHCR linasema kuwa Yemen inawahifadhi wakimbizi wapatao 238,000 kutoka Somalia. Mwandishi wa BBC Africa Mary Harper anasema wazo la Yemen kufikiria kuwa na kambi za wakimbizi nchini Somalia si la kawaida kwa kuwa ni kawaida kwa raia nchini humo kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya mara kwa mara hali ambayo haiwezi kuwa eneo zuri kwa wakimbizi kuhifadhiwa.
chanzo bbc.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni