Ripoti kutoka Yemen zinasema kuwa
waasi wa Houthi wameondoka nyumba ya rais waliokuwa wameiteka katika mji
muhimu wa kusini wa bandari ya Aden baada ya mshambulizi ya ndege za
taifa la saudia kulenga eneo hilo.
Wapiganaji walio watiifu kwa
rais Abd Rabbuh Mansur Hadi wanasema kuwa wamepokea zana za kijeshi
zilizoangushwa kutoka ndege za kijeshi za saudia wakati ambapo mapigano
yanaendelea katika mji huo.China imewaondoa zaidi ya raia wa kigeni 200 kutoka bandari hiyo.
Makumi ya raia yameripotiwa kuuawa siku chache zilizopita katika mapigano ya Aden.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni