Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Ijumaa, 3 Aprili 2015

ZIMBABWE; ZANU-PF CHAMTIMUA BIMUJURU.

Bi Joice Mujuru
Aliyekuwa makamu wa rais nchini Zimbabwe Joice Mujuru amefukuzwa katika chama tawala ZANU-PF.
Chama hicho kinasema alipanga njama za kumuondoa mamlakani rais Robert Mugabe mbali na kukiharibia jina chama hicho- madai ambayo ameyakana hapo mbeleni .
Bi Mujuru alipigana vita vya Guerilla pamoja na Mugabe miaka ya sabini dhidi ya uongozi wa weupe na alionekana kama mrithi wake,kabla ya kukosana naye mwaka uliopita swala lililomfanya kufutwa kazi kama makamu wa rais mnamo mwezi Disemba.
Waandishi wanasema alishtumiwa sana na mke wa Mugabe, Grace ambaye anaongoza wanawake katika chama hicho.
CHANZO BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni