Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Ijumaa, 3 Aprili 2015

WAKWE WANYWESHA MKOJO KWA MWAKA MMOJA.

Machoni anatazamika, lakini moyoni alikuwa hana raha.
Mwanamke mmoja nchini India amekuwa na mazoe na tabia kujengeka ya kukojolea vikombe vya wakweze kila iitwapo leo kwa muda wa mwaka mmoja ,zake zilitimia baada ya kufumwa na mama mkwe wake jikoni akiwa amekinga buli la chai anakojoa ndaniye.
Chanzo kisa na sababu ya kadhia hiyo kutokea ni wakweze kumpiga marufuku mtoto wao wa kiume kufanya kazi za nyumbani na ndipo mkwe huyo alipoamua kujilipiza kisasi kwa kukojolea vikombe vya wakweze kwa zaidi ya mwaka mmoja.Rekha Nagvanshi, mwenye umri wa miaka 30,alikuwa akiishi nyumba moja yeye na mumewe Deepak,mwenye miaka 34, katika wilaya ya Indore jimbo la Madhya Pradesh,pamoja na wakweze .
Mwanamke huyo alidai kwamba ingekuwa bora angeishi na nduguze kuliko kuishi kwa wakeze,na alisema kwamba hakuwa na furaha namna ndoa yake ilivyoendeshwa na alikuwa akijihisi anatendewa visivyo na hapati matunzo muafaka.Rafiki wa mwanamke huyo , Alia Kohli, mwenye umri wa miaka 32, alisema kwamba rafikiye hakuwa na furaha na ndoa yake tangu siku ya kwanza ya harusi na mumewe alikuwa akimtenda kama mtumwa na mwanamke huyo ameamua kuwa imetosha.
Lakini chakushangaza baada ya kuondoka kuelekea kwa wazazi wake , mara aliomba kurejea ukweni ati tu kwasababu ya majaaliwa ya mtoto wao wa kike aliye na umri wa miaka minne ili aendelee kumpa malezi yake,na alipo rejea kwa wakweze aliweka masharti ya mumewe kumpikia chakula,kumkandakanda miguu yake na kumfulia nguo zake zote lakini wazazi wa kijana huyo hawakuridhishwa na masharti hayo ,hivyo waliweka mpango wa kukomesha masharti hayo.

Tabasamu usoni rohoni anakereketwa
Mume wa mwanamke huyo Deepak anasema kwamba yeye alikuwa radhi na masharti ya mkewe lakini wazazi wake walimjia juu na kumsema kwamba hiyo haikubaliki kwani anamshurtisha mtoto wao kama mtumwa.
hata hivyo inaelezwa kwamba,wazazi wa mwanaume huyo walikuwa na kawaida ya kuwatembelea watoto wao mara moja kwa wiki, kitendo kilichokuwa kikimkera mno mkamwana wao na akaamua kuwatenda, wazazi walipogundua hila yake walisema kwamba walijua mkwe wao hawapendi lakini hawakufikiria kwamba anaweza kuwatenda namna hiyo,maana alikuwa akitabasamu na kuwapa chai nao waliipokea,lakini siku moja mamake Deepak niliingia ghafla jikoni na kumfuma mkwe akikojolea birika ya chai.
wazazi hao mke Suraj na mume waliamua kwenda kutoa taarifa polisi ,na huko wakatwambia masuala ya namna hiyo hawashughuliki nayo,wazazi wa mwanaume huyo wakadai sheria ichukue mkondo wake maana si jambo rahisi kwa mwaka mmoja mtu akojolee birika yenye chai na aachiliwe hivi hivi, wanataka haki itendeke.
Kufuatia kisanga hicho imejulikana familia iko mbioni kulipeleka mahakamani suala hilo na kwamba Rekha na mumewe Deepak wametengana.
CHANZO BBC.

WAANDANA DHIDI YA AL-SHABAAB GARISSA.


Maandamano Garissa 
Wananchi wa mji wa Garissa nchini Kenya wamefanya maandamano kupinga vitendo vya kundi la Al Shabaab, lililoshambulia chuo kimoja kikuu mjini humo na kuwaua watu 147 wengi wao wakiwa wanafunzi hapo jana.
Waandamanaji pia wameelezea kutoridhika na vyombo vya usalama nchini humo wakisema havikuchukua hatua za kutosha kutoa ulinzi kwa waliouawa na kwa raia wengine kwa jumla.
Wazazi, jamaa na marafiki wa wanafunzi waliouawa katika chuo kikuu cha Garissa wamekuwa wakiendelea kuwasili katika eneo hilo kuitambua miili ya wapendwa wao.
Waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu .

Garissa
Serikali ya Kenya imekuwa ikiwasafirisha manusura wa shambulio hilo kwa mabasi kuelekea makwao huku miili ya waliouawa ikisafirishwa mjini Nairobi.
Wakati huo huo rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamoud, amesema Somalia na Kenya zinafaa kuimarisha uhusiano wao katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Tamko hilo linajiri siku moja baada ya shambulio hilo la Alshaabab katika chuo kimoja kikuu mjini Garrisa.
chanzo bbc.

SIMBA SC YAPATA PIGO, WANACHAMA WAKE 7 WAFA AJALINI

 
Wanachama Saba (7) wa klabu ya Simba ya Dar es salaam kutoka tawi la Mpira na Maendeleo (maarufu kama Simba UKAWA) ambalo limewahi kutangazwa kufutwa wamefariki dunia katika ajali ya basi mkoani Morogoro.
Wanachama hao wakiwa katika basi lao walikuwa wakielekea Shinyanga kwa ajili ya kuipa nguvu Simba ambayo inatarajiwa kushuka katika dimba la CCM Kambarage kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kesho..
Vifo hivyo vimefikia 7 baada ya watano kufa palepale na wengine wawili waliokuwa majeruhi kufariki katika hospitali ya mkoa wa Mororgoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Leonard Paul amethibitisha habari hizi na kusema kuwa majeruhi wamebaki 13 na kufanya vifo kufikia saba hadi majira ya saa 2 usiku wa April 03.

Alhamisi, 2 Aprili 2015

GOA HAWATAKI WAPENZI KUBUSIANA HADHARANI.

sherehe za hadhara.
Kijiji kimoja nchini India kilichoko pwani ya Goa kimeweka sheria ya kuzuia wanandoa ama wapenzi kubusiana hadharani ,kwa madai kuwa wenyeji wa maeneo hayo hawapendi tabia za kimagharibi kwenye eneo lao.
Bunge la kijiji hicho liitwalo Salvador-de-Mundo,ambalo liko kilomita nane Kaskazini ya mji wa Goa kwenye mji wa Panaji, azimio hili limepitishwa mapema wiki hii likiwaonywa wenye kufanya sherehe za hadhara wasijisahaulishe sheria hiyo na kuoneshana mahaba hadharani.
Tumeamua kulipitisha azimio hili baada ya kupokea malalmiko kutoka kwa wanakijiji juu ya watu wanaobusiana hadharani.hii ndio njia pekee ya kulimaliza suala hili anasema chifu msaidizi wa kijiji hicho Reena Fernandes .
Bibi huyo ambaye ni chifu msaidizi ameongeza kwamba malalamiko yao waliyapeleka kwa viongozi wa kijamii lakini hawakupata mrejesho wala hatua zozote kuchukuliwa na hivyo wakaamua kuchukua sheria mikononi na kupasisha azimio la marufuku ya kunywa pombe hadharani na kupiga muziki hadharani kwa sauti kubwa.
Hata hivyo ,amekataa kuzungumzia chochote juu ya hatua za adhabu zitakazo chukuliwa kwa wataovunja sheria hiyo .
Mwanakijiji mmoja Savio Rebeiro amesema kwamba tumezizuia pwani zinazovutia utalii,maana mara kwa mara huwa tunashuhudia wapenzi wawili wafanyao matendo yanayo tukera .

rahaje???????
Ukanda huo wa bahari ya hindi wenye biashara kubwa ya uvuvi kwa sasa wamesambaza mabango yenye ujumbe wa elimu juu ya katazo hilo.
Pwani za Goa zimejaa mchanga zenye mvuto wa kipekee kwa mamilioni ya watalii kutoka Magharibi na katazo hilo limetia doa utalii.
Naye waziri mkuu Narendra Modi mwenye asili ya Kihindu wa chama cha Bharatiya Janata wiki hii aliweka marufuku ya wanawake waajiriwa kuvaa suruali za jinzi na singilendi katika ofisi za serikali.
Mwaka uliopita waziri wa Goa alitaka itungwe sheria ama amri ya katazo la uvaaji bikini katika pwani zote na alipokea upinzani mkubwa kutoka kwa jamiina tasnia ya utalii.
CHANZO BBC.

KESI YA KUJIUNGA NA UGAIDI YAONGEZEKA.

Wapiganaji wa kundi la Islamic State
Zaidi ya wapiganaji wa kigeni elfu ishirini na watano kutoka mataifa mia moja walisafiri kwa nia na malengo ya kujiunga na makundi ya kijeshi kama al-Qaeda na Islamic State (IS), taarifa ya umoja wa mataifa imeeleza hayo.
Taarifa hiyo imeeleza pia kwamba wapiganaji wageni ulimwenguni idadi yao imeongezeka mpaka kufikia asilimia sabini na moja katikati ya mwaka 2014 na march mwaka huu.
Nchi za Syria na Iraq ndizo nchi zinazolengwa kwa ukaribu zaidi na ndicho kitovu cha vijana wanaomaliza mazomo yao na kugeuka kuwa wenye msimamo mkali wa kidini.
Na pia taarifa hiyo imebainisha kuwa endapo kundi la IS lingeshindwa nchini Syria na Iraq,sasa wapiganaji hao kutoka nchi za kigeni wamesambaa ulimwenguni .
Nalo baraza la usalama la umoja wa mataifa liliwaomba wataalamu wa masula ya kijeshi miezi sita iliyopita kuchunguza vitisho vya askari wa kigeni wanaojiunga na kundi la Is na makundi mengine ya kigaidi.
Katika ripoti iliyowasilishwa kwenye baraza hilo mwishoni mwa mwezi uliopita ,na wataalamu wakaeleza kuwa ongezeko la wapiganaji wa nchi za kigeni zinazidi kuongezeka kulinganisha na muongo mmoja uliopita .
Maelfu ya wapiganaji wa kigeni ambao hufanya safari hadi nchini Syria ,Falme za Kiarabu na Iraq huko hufanya makao na kufanya kazi na kumalizia masomo ya elimu ya juu kwa wenye msimamo mkali kamalivyowahi kutokea kwatika nchi ya Afghanistan miaka ya 1990 .
Syria na Iraq inasemekana ina makaazi elfu ishirini na mbili kwa wapiganaji hao wa kigeni ,pia nchini Afghanistan makaazi elfu sita na mia tano na maelfu ya makaazi nchini Yemen, Libya, Pakistan na Somalia.
CHANZO BBC.

KANISA KATOLIKI LINAUTAZAMAJE USHOGA??

Raymond Burke
Kadinali Raymond Burke mwenye asili ya Marekani ameenguliwa na Papa Francis katika wadhifa wake wa mwenyekiti wa bodi katika kanisa katoliki,ametoa onyo kwamba kuna viashiria vya kanisa hilo kuupigia chapuo ushoga, kauli hii Burke aliiotoa wakati alipokuwa akihojiwa na tovuti moja ya Italy ya La Nuova Bussola Quotidiana mara baada tu ya kuenguliwa kwenye wadhifa wake.
Mwandishi wa BBC anasema hii ni ishara nyingine ya jinsi viongozi wa dini waandamizi wanavyochukulia hatua juu ya masuala kama vile ushoga na talaka , wakati wengine wanatakiwa kuyachukulia mambo kwa utuvu na uangalifu wa hali ya juu.
chanzo bbc.

HABARI ZA MOJA KWA MOJA KUTOKA GARISSA

Idhaa yako ya kiswahili ya BBC imekuandalia ukurasa wa habari za moja kwa moja kufuatia shambulizi la chuo kikuu nchini Kenya.

14.00pm:Kwa ufupi

wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa
Takriban watu 15 wanaodaiwa kufinika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.
Watu hao wanaodaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.
Hatahivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja unusu.


Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho waliosalimika
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema kuwa walinzi wawili waliuawa katika lango la chuo hicho huku maafisa wawili wa polisi waliokuwa wakilinda chuo hicho pamoja na wanafunzi wakijeruhiwa.
Walioshuhudia wanasema kuwa kumekuwa na majeruhi mengi ndani ya chuo hicho.
Mwandishi wetu anasema kuwa wapiganaji hao bado wako ndani ya chuo hicho na wamewateka nyara watu kadhaa.

Wanafunzi waliotoroka shambulizi mjini Garissa Kenya
Jeshi la Kenya KDF ,maafisa wa polisi na amabulansi wamefika katika eneo la tukio na sasa wameingia ndani ya majengo ya chuo hicho ambapo kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya washambuliaji na maafisa wa jeshi.


13.40pm:Waislamu na wakristo waliotekwa ndani ya Jumba hilo la Chuo kikuu cha garissa wamedaiwa kutawanywa kabla ya waislamu 15 kuwachiliwa huru kulingana na msemaji wa kundi hilo la Alshabaab.

13.35pm:Serikali ya kenya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulihutubia taifa kufuatia shambulizi hilo la chuo kikuu cha Garrisa mapema leo.

13.30pm:Alshabaab:

Maafisa wa Polisi wa kenya
kundi la wapiganaji wa Alshabaab limesema kuwa liko ndani ya Chuo hicho kikuu na limewatawanya waislamu na wakristo

13.20pm:Wapiganaji wamedaiwa kuwateka nyara wanafunzi na kuwaua watu 14 katika chuo hicho kulingana na wafanyikazi wa msaada na maafisa wa polisi.Takriban watu 65 wengine wamejeruhiwa baada ya washambuliaji kuvamia chuo hicho.Vituo vya habari nchini kenya hatahivyo vinaiweka idadi hiyo kuwa watu 16.

13.05pm:Idadi ya watu waliouawa kufuatia shambulizi la wapiganaji wa kundi la alshabaab imefikia 14

13.03pm:Al shabaab


Alshabaab lakiri kutekeleza shambulizi 

Kundi la wapiganaji wa Al-shabaab limekiri kutekeleza shambulizi katika chuo kikuu cha Garissa Kaskazini mashariki mwa Kenya huku likiwaua watu 14

12.47pm:Wanafunzi

 
wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya
Chuo hicho cha Garissa kina takriban wanafunzi 1000, na wafanyikazi wengine.


12.30pm Wanafunzi:
 

 Wanafunzi waliodaiwa kutoroka
Baadhi ya wanafunzi wamedaiwa kutoroka kutoka mabweni waliokuwa wakilala


12.20pm:Wapiganaji

Wapiganaji
Wapiganaji hao wanaodaiwa kuwa watano wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo la Chuo kikuu .


12.18pm:Kenya Red Cross
 
Maafisa wa polisi wakikabiliana na wapiganaji huko Garissa kenya
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya linasema kuwa watu 30 wamejeruhiwa huku wanne kati yao wakiwa na majeraha mabaya..Kwa sasa shirika hilo linawasafirisha madaktari katika eneo hilo.
11.30am Idadi ya watu waliouawa kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya imefikia watu sita huku wengine 29 wakidaiwa kujeruhiwa.
 CHANZO BBC.