Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatatu, 29 Desemba 2014

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI AFUNGUKA KUHUSU MAFUTA.


Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo bado inayowauzia wananchi wake mafuta kwa bei ya juu licha ya kuwa bei ya mafuta katika soko la dunia kushuka kwa zaidi ya asilimia 50.
Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ameyasema hayo wakati akiongea na Wananchi wa Halmashauri ya mamlaka ya mji mdogo wa Kyela na kusema kuwa kumekuwepo na bei kubwa ya mafuta nchini ikilinganishwa na nchi nyingine.

Jumapili, 28 Desemba 2014

HII NI LAANA,,,,SI BURE.NJEMBA LAJIONGEZA MAKALIO.

BASI LA ZUBERI LAGONGANA USO KWA USO NA COSTA

Basi la Zuberi no 3,limegongana uso kwa uso na costa hakuna alietoka kwenye costa na imekwisha nyang'anyang'a.hali hii imepelekea waliokuwa kwenye gari nyingine kushuka na kuokoa majeruhi.nimbele kidogo ya Singida mjini.

UPEPO WAKWAMISHA UOKOAJI MELI ILIYOZAMA


Meli ya uokoaji 
Waokoaji wamekuwa wakipambana na upepo mkali pamoja na mawimbi ya bahari gizani kuwakoa karibu abiria 300 ambao wamekwama ndani ya ferry moja ya Italia iliyokuwa imeshika moto kwenye bahari ya Adriatic.
Maofisa nchini Italia wanasema kuwa oparesheni ya uokoaji itandelea.Hadi sasa watu 190 wamekolewa kutoka kwa ferry hiyo.
CHANZO BBC

FILAMU YA INTERVIEW YATIKISA MTANDAONI

Filamu ya Interview
Kampuni ya Sony Picutues inasema kuwa - the interview - ambayo ni filamu yenye utata ya dhihaka kuhusu njama ya kumuua kiongozi wa korea kasakzini Kim Jong un imekuwa yenye mafanikio zaidi mtandaoni.
Kampuni hiyo inasema kuwa filamu hiyo imenunuliwa na pia kukodishwa zaidi ya mara milioni mbili kwa muda wa siku nne tangu iwekwe kwenye mitandao.
Sony iliahirisha mpango wake wa filamu baada ya komputa za kampuni hiyo kudaiwa kuingiliwa na wadukuzi,huku Korea Kaskazini ikihusishwa katika udukuzi huo.
CHANZO BBC

NDEGE ILIYOPITEA JANA YAENDELEA KUTAFUTWA


Airasia iliotoweka
Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.
Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.
CHANZO BBC

WATOTO WAZUIWA KUITEMBELEA ISRAELI

Watoto waliotekwa Gaza ndani ya Basi 
Kundi la Hamas limewazuia kundi la watoto kutoka ukanda wa Gaza wengi wakiwa ni wale waliowapoteza wazazi kwenye vita vya hivi majuzi kati ya Hamas na Israel waliotaka kuitembelea Israeli katika ziara ambayo waandalizi wake wanasema ililenga kuleta uwiano. Msemaji wa Hamas anasema kuwa ziara hiyo ilizuiwa ili kulinda tamaduni ya watu wa ukanda wa Gaza.
Wapiganaji wa kundi la Hamas wamezuia kundi la watoto kutoka Gaza wengi wao wakiwa ni wale ambao wazazi wao waliuawa katika vita.
Wanaharakati wa masuala ya Amani waliowasaidia watoto hao kufanya safari hiyo wamesema kuwa mamlaka ya Gaza waliruhusu watoto hao kufanya safari yao lakini wakabadili msimamo wao baadae.
chanzo bbc