Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 31 Desemba 2014

RAIS WA GAMBIA ARUDI NYUMBANI


Rais wa Gambia Yahya Jammeh
Ripoti kutoka Gambia zinasema kuwa rais Yahya Jammeh amerudi nchini humo kutoka ziara ya ughaibuni kufuatia njama ya kutaka kumpindua.
Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.
Haijulikani ni wapi rais Jammeh alikokuwa huku ripoti zikidai kuwa alikuwa nchini Ufaransa na wengine wakisema alikuwa Dubai.
Mkuu wake wa itifaki ameiambia BBC kwamba kila kitu kiko shwari katika mji mkuu.
CHANZO BBC

MFALME ABDULLAH WA SAUDI ALAZWA


Mfalme Abdullah wa saudia alazwa hospitalini
Mfalme Abdullah wa Saud Arabia amelazwa hospitalini ili kufanyiwa ukaguzi.
Taarifa kutoka kwa makao ya mfalme huyo haikutoa maelezo yoyote kuhusu hali yake.
Soko la hisa la Saudia lilianguka baada ya habari hizo kutangazwa katikan runinga ya taifa.
Mfalme Abdullah aliye na umri wa miaka 90 ametawala ufalme wa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu mwaka 2005.
CHANZO BBC

RAIS WA GAMBIA ARUDI NYUMBANI KWAO


Rais wa Gambia Yahya Jammeh
Ripoti kutoka Gambia zinasema kuwa rais Yahya Jammeh amerudi nchini humo kutoka ziara ya ughaibuni kufuatia njama ya kutaka kumpindua.
Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.
Haijulikani ni wapi rais Jammeh alikokuwa huku ripoti zikidai kuwa alikuwa nchini Ufaransa na wengine wakisema alikuwa Dubai.
Mkuu wake wa itifaki ameiambia BBC kwamba kila kitu kiko shwari katika mji mkuu.
CHANZO BBC.

Jumanne, 30 Desemba 2014

KITU KINA LOADING.........


UONGOZI WA rayshughuli.blogspot.com UNAWATIKIA KILA LA HERI KATIKA SHEREHE ZA KUUAGA MWAKA 2014.



2014,,,,UNASEMA HIVI......


MICHAEL VAN GERWEN ATINGA NANE BORA


 Michael Van Gerwen
Mchezaji wa mchezo wa Vishale Michael van Gerwen,amefanikiwa kuingia hatua ya nane bora katika michezo ya dunia kwa kumfunga Terry Jenkins kwa mabao 4-1
Katika michezo mingine Robert Thornton pia aliibuka kidedea kwa kumchapa Benito van de Pas kwa mabao 4-0 na atachuana na Van Gerwen katika hatua ya robo fainali.
Raymond van Barneveld alifanikiwa kuingia robo kwa kupata ushindi wa 4-3 dhidi ya mpinzani wake Jamie Caven.
Huku Stephen Bunting akishinda kwa ushindi wa 4-1 mbele ya James Wade, Mwingereza Smith alipata ushindi licha ya kutanguliwa kwa 2-0 kwenye awamu ya kwanza na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Brendan Dolan.
Mchezaji wa Uholanzi Vincent van der Voort alimaliza kwa kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 kwa kumtwanga Max Hopp toka Ujerumani.
CHANZO BBC.

KOMBE LA MAPINDUZI KUANZA KUANZA JANUARI MOSI


Timu ya Kmkm ya Zanzibar moja kati ya washiriki
ichuano ya kombe la mapinduzi kuanza kutimua vumbi Zanzibari kuanzia januari mosi mpaka Januari 13 mwakani.
Hii itakua ni mara ya tisa kufanyika tangu ianzishwe kuenzi Mapindunzi ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12, 1964.
Timu zinazotarajiwa kushiriki michuano hiyo ni pamoja na Yanga Sc, Azam Fc,Simba Sc na Mtibwa Sugar.
Wenyeji watawakilishwa na mabingwa wa Zanzibar KMKM, Police FC, JKU, Mtende Rangers na Shaba FC.
KCC FC ya Uganda watashiriki pia michuano hiyo wakiwa ni mabigwa watetezi wa kombe hilo.
Timu waalikwa toka nchini kenya zilizoalikwa kushiriki michuano hii zimejitoa.

KOBE BRYANT AANZA VIBAYA NBA


Kobe Brayant
chezaji nguli wa mchezo wa kikapu Nchini Marekani Kobe Bryant amerejea vibaya katika kikosi chake cha LA Lakers kwa kukubali kichapo cha vikapu 116 -107 – toka kwa Phoenix Suns.
Kobe alikua anareje uwanja ni baada kukosa michezo mitatu iliyopita, alifunga pointi 10 ribaundi 8 na akisaidia kutoa pasi 7 za mwisho za vikapu.
Goran Dragic aliifungia Phoenix Suns pointi 24 na Eric Bledsoe akiongeza pointi 22
Matokeo mengine ya NBA yalikua Cleveland Cavaliers 80 - 103 Detroit Pistons ,San Antonio Spurs 110 - 106 Houston Rockets ,Dallas Mavericks 112 - 107 Oklahoma City Thunder, Denver Nuggets 102 - 116 Toronto Raptors ,Portland Trail Blazers 101 - 79 New York Knicks.
CHANZO BBC

TUZO ZA CAF KUTOLEWA JANUARI


Pierre-Emerick Aubameyang
Shirikisho la soka barani Afrika CAF litatoa tuzo kwa wanamichezo bora Januari 8 huko Lagos Nigeria.
Kiungo wa Gaboni Pierre-Emerick Aubameyang, golikipa Vincent Enyeama wa Naijeria na kiungo Yaya Toure ndio wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2014.
Wanaowania Tuzo za uchezaji bora kwa wachezaji wa ndani ya Afrika
Akram Djahnit (Algeria) El Hedi Belamieri( Algeria)Firmin Mubele Ndombe (DR Congo)
Kwa upande wa wanawake wanaowania tuzo hizo ni
Annette Ngo Ndom (Cameroon) Asisat Oshoala (Nigeria) Desire Oparanozie (Nigeria)
Wanaowania kwa upande wa chipukizi
Asisat Oshoala (Nigeria) Fabrice Ondoa (Cameroon)Uchechi Sunday (Nigeria)
Wanaowania tuzo ya kipaji kinachochipukia ni
Clinton N’jie (Cameroon) Vincent Aboubakar (Cameroon) Yacine Brahimi (Algeria)
makocha wanaowania tuzo hizo
Florent Ibenge (DR Congo) Kheireddine Madoui (ES Setif) Vahid Halilhodžić (kocha wa zamani wa Algeria)
Timu zinazowania tuzo ya timu bora ya mwaka ni
Algeria, Libya, Nigeria
Timu bora ya wanawake ya Mwaka ni
Cameroon, Nigeria, Nigeria U-20
Klabu bora ya Mwaka
Al Ahly (Egypt) AS Vita (DR Congo) ES Setif (Algeria)
Huku Rais wa Tp Mazembe Moise Katumbi Chapwe akitarajiwa kupewa tuzo ya kiongozi bora wa michezo wa mwaka.
CHANZO BBC.

KASHFA YA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU 2014


Wanariadha wa Tanzania wakiwa mazoezini
Chama cha riadha Tanzania (AT) kimesema mwaka 2014 umekuwa na mafanikio katika kudhibiti utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu kwa wanamichezo wake licha ya kufanya vibaya katika michuano ya kimataifa kama vile michezo ya Jumuiya ya Madola iliyochezwa Glasgow, Scotland ambapo Tanzania haikupata medali.
Wakati Tanzania ikiwa haina mwanariadha aliyekamatwa na kashfa ya utumiaji madawa ya kuongeza nguvu michezoni mwaka 2014, hali imekuwa tofauti kwa majirani Kenya ambayo imeripotiwa kuwa na wanariadha 26 waliokamatwa na kuhusishwa na utumiaji licha ya kufanya vizuri kimataifa.
“ Tulitoa elimu ya kutosha kwa wanariadha wetu na siku zote tuliwaeleza kuwa mazoezi na jitihada ndio siri pekee ya ushindi na si utumiaji wa madawa”, alisema mtendaji mkuu wa riadha Tanzania, Suleiman Nyambui.
Nyambui, ambaye ni mmoja kati ya wanariadha wawili wa zamani nchini Tanzania walioweka rekodi ya kushinda medali mbili katika michuano ya Olimpiki tangu nchi ilipopata uhuru wa kisiasa mwaka 1961, alisema mwaka juzi ni mwanariadha mmoja tu aliyekamatwa katika utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu.
“Tunajivunia usafi wa wanariadha wetu kwa mwaka 2014”.
“Kesi za utumiaji wa dawa nchini mwetu zinapungua kila miaka inavyokwenda”, alisema Nyambui.
Wakati Kenya ikiongoza dunia katika mbio, ripoti kutoka magazeti ya Kenya zinasema kuwa wachezaji 26 akiwamo mshindi mara mbili wa mbio za Chicago na Boston, Rita Jeptoo ambaye vipimo vilionesha ametumiwa dawa.

AZAM WATAMBA KUIFUNGA KCC YA UGANDA


Timu ya Azam
Mabingwa watetezi wa soka Tanzania bara, Azam FC wamepania kuwafunga KCC ya Uganda katika mechi ya ufunguzi ya kombe la Mapinduzi ya Zanzibar linakaloanza January 1 visiwani Zanzibar.
Kulikuwa na tetesi kuwa mabingwa hao wangeweza kukutana na wapinzani wao wa kombe la klabu bingwa Afrika, El-Merreikh ya Sudan, ambao waliombwa kuwa sehemu ya timu shiriki katika moja ya mechi ya michuano hiyo., Lakini mpaka hivi punde, taarifa zilisema kuwa El-Merreikh hawatashiriki kutokana na waandaaji kushindwa kukidhi baadhi ya mahitaji yao.
Iwapo mabingwa hao wa kombe la shirikisho la Afrika 2014/2015, El-Merreikh watashiriki, basi msisimko wa michuano hiyo utaongezeka.
“Tumejipanga vya kutosha na kuwa mabingwa”.
“Tuna taarifa kuwa El-Merreikh watashiriki, kama ni kweli itakuwa ni kipimo tosha baina yetu kabla ya kucheza hapo mwakani (kati ya Januari 13, 14 au 15) katika mechi za hatua za awali za michuano ya klabu bingwa Afrika”, alisema msemaji wa klabu ya Azam, Jaffar Iddi.
Timu za Yanga, Simba na Mtibwa sugar zitaungana na Azam kutoka Tanzania Bara kushiriki michuano hiyo yenye lengo la kuadhimisha Mapinduzi tukufu ya Zanzibar yaliyotokea mwaka 1964.
Timu wenyeji ni KMKM, Mafunzo, Mtende Rangers na Shaba wakati kulikuwa na taarifa kuwa Ulinzi ya Kenya nayo ilitegemewa kushiriki lakini haitasafiri kwenda Zanzibar.

AZIMIO KUHUSU PALESTINA LAKATALIWA


Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limekataa azimio lililoandaliwa na Palestina ambalo limewasilishwa na Jordan linalopendekeza kusitishwa kwa mpango wa Israel wa kuyakalia maeneo ya Palestina kwa miaka miaka mitatu.
Jordan iliwasilisha azimio hilo baada ya kukubaliwa na nchi 22 za kiarabu ikiwemo mamlaka ya Palestina.
Kura tisa zilihitajika ili kupitisha azimio hilo lakini azimio hilo lilipigiwa kura nane pekee.
Nchi mbili zilipiga kura ya hapana kupinga azimio hilo ambazo ni Australia na Marekani zilizokataa mpango huo wa mwisho na kusema hautasaidia katika masuala ya usalama wa Israel.
Nchi tano hazikupiga kura ambazo ni Uingereza, Lithuania, Nigeria, Jamuhuri ya Korea na Rwanda, huku Urusi, China, Ufaransa, Argentina, Chad, Chile, Jordan na Luxembourg zikilipigia kura ya ndio azimio hilo.
CHANZO BBC.

NDEGE ILIYOPOTEA;UTAFUTAJI WACHELEWA.


Ndugu wa abaria waliopotea kwenye ndege ya AirAsia wakilia kwa uchungu
Hali mbaya ya hewa imechelewesha zoezi la anga na majini la utafutaji wa ndege ya AirAsia aliyoanguka ikiwa na watu 162 baada ya kuwepo kwa dhoruba katika pwani ya eneo la Borneo siku ya jumapili.
Kufuatia kupatikana kwa vipande vya mabaki ya ndege hiyo siku ya jumannne, kiongozi wa taasisi ya uokoaji na utafutaji amesema miili mitatu imepatikana hadi sasa kutoka katika eneo la bahari ya Java.
Wapiga mbizi wa kikosi cha maji cha jeshi wanatarajiwa kuanza kutafuta miili na kinasa sauti cha ndege hiyo katika kina cha chini cha maji katika eneo linalosadikiwa ndipo ndege hiyo ilipoangukia.
Ndege hiyo ilipotea ikiwa safarini ikitokea mji wa Surabaya nchini Indonesia kuelekea nchini Singapore.
chanzo bbc.

TIZAMA PICHA ZA MAFURIKO YALIYOTOKANA NA MVUA YA JANA ILIYONYESHA KWA SAA 2.JE IKINYESHA KWA SIKU 3MFULULIZO ITAKUWAJE ?

KIWANDA CHA JUICE CHAFUNGIWA


Shirika la viwango nchini TBS limefanya ukaguzi wa kushtukiza na kufungia kiwanda cha Devideic Group kinachotengeneza juisi aina ya Into kilichopo Kihonda manispaa ya Morogoro kwa kuuza juice zenye vimelea vya wadudu.

TANZANIA MWENYEJI MPIRA WA UFUKWENI


Mazoezi ya wavu yakiendelea
Tanzania imechaguliwa na shirikisho la mpira wa wavu Afrika (CAVB) kuwa wenyeji wa michuano ya kanda ya Tano ya Beach Volleyball ( mpira wa wavu ufukweni).
Michuano hiyo itakayofanyika kuanzia February 16-18 mwakani itakuwa ni sehemu ya kufuzu kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika Rio de Janeiro, Brazil mwaka 2016.
Mkurugenzi wa Kamisheni ya wavu ufukweni, Muharrami Mchume amesema wapo tayari kwa uwenyeji na kuongeza kuwa Kenya, Burundi, Somalia, Ethiopia, Djibouti na wenyeji Tanzania ndio nchi zitakazoshiriki.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa wenyeji wa michuano hiyo.
Mchezo wa mpira wa wavu sio maarufu sana nchini Tanzania licha ya kuwa na fukwe nyingi za bahari.
CAVB ipo katika jitihada za kuendeleza mchezo huo wa ufukweni na hivi karibuni liliendesha semina nchini Tanzania ambayo ilishirikisha washiriki kutoka zaidi ya nchi tano katika jitihada za kuukuza mchezo huo katika nchi za kanda ya tano hasa mashuleni.
Michuano hiyo inategemewa kufanyika katika fukwe za beach ya Mbalamwezi jijini Dar es Salaam.

FA KUMUADHIBU CISSE-




Mshambuliaji wa Newcastle United Papiss Dembaba Cisse.
Chama cha Soka England(FA) kimemfungulia mashitaka mshambuliaji wa Newcastle United Papiss Cisse.
Cisse amefunguliwa mashitaka kwa kosa la kumpiga kiwiko Beki Seamus Coleman wa klabu ya Everton.
Refa wa Mechi hiyo Craig Pawson hakuona tukio la Cisse kumpiga na kiwiko Coleman katika mchezo wa ligi kati ya Newcastle na Everton.
Meneja wa Everton, Roberto Martinez, akiongea baada yamchezo alisema: “Cisse alikua na bahati kutokutolewa mchezoni, kama hatutaki kuona haya Uwanjani, yasiruhusiwe. Alipaswa kupewa Kadi Nyekundu.”
Ikiwa atapatikana na hatia Cisse atakosa michezo mitatu ya

BARCLONA YAFUNGIWA KUSAJILI MPAKA 2016


      Timu ya Barcelona
Shirikisho la soka dunia FIFA limeitupilia mbali rufaa iliyokatwa na klabu ya Barcelona kuhusu kuizuia kusajili kwa kukiuka kanuni ya usajili.
Barca walifungiwa kwa miezi 14 kusajili baada ya kufanya makosa kwa kusajili kinda wa chini ya miaka 18, Ikiwa ni kinyume na kanuni za usajili za Fifa.
Kwa maamuzi haya timu hii haitakua na uwezo wa kusajili mchezaji mpya mpaka Januari 2016.Barcelona wantarajia kukata rufaa tena maamuzi haya ya Fifa kwenye mahakama ya usuhuhishi michezoni(Cas).
Miamba hiyo ya soka ilifanikiwa kuwasajili mshambuliaji Luis Suarez , mabeki Thomas Vermaelen Jeremy Mathieu golikipa Claudio Bravo na kiungo Ivan Rakitic mwanzoni mwa msimu baada ya baada ya kupewa ruhusa maalumu na Fifa.
CHANZO BBC.

MTOTO WA MIAKA MINNE ATEKWA MWANZA


Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Valentino Mlowola
Nchini Tanzania katika Kijiji cha Ndami, tarafa ya Mwamashimba wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza watu wasiofahamika wamevunja nyumba na kumteka mtoto mwenye ulemavu wa ngozi maarufu kama albino na kutoweka naye.
Watu hao walivamia nyumba ya wazazi wa mtoto Pendo Emmanuel, mwenye ulemavu wa ngozi wakiwa na mapanga na kisha kutoweka naye gizani baada ya kuwazidi nguvu wazazi wake.
Emmanuel Shilinde mzazi wa mtoto huyo ameieleza polisi kuwa majira ya saa nne usiku watu wawili waliuvunja mlango wa nyumba yake kwa jiwe wakamchukua mtoto kwa nguvu kisha wakakimbilia gizani kwa pikipiki.
Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi mkoani mwanza Valentino Mlowola , ameitaarifu BBC kuwa leo ni siku ya tatu na polisi bado ina matumaini ya kumpata akiwa hai motto huyo, kwa kuwa bado hawajaupata mwili wake akiwa amepoteza uhai. Msako unaendelea na tayari kuna watu watano wanazuiliwa na polisi ili kusaidia kufahamu mtoto huyo yuko wapi.
Takwimu za kuanzia mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wamepata ulemavu mwingine wa kudumu.

MIILI 40 YAOPOLEWA BAHARINI


Sala za kuwaombea waliokuwa wasafiri katika ndege hiyo zinaendelea
Kufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At ,miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea.
Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.Na taarifa kutoka serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa imebeba abiria mia moja na sitini na wawili ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore,ilipotea siku ya Jumapili.
Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu,na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha nchi kavu na baharini.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.
Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini iliopolewa na meli ya kivita .
Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia Fernandes ali ingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi .
Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.
CHANZO BBC

Jumatatu, 29 Desemba 2014

XMASS,CHIUJANINUNUIA NGUO YA CHUKUKUU.CHACHA MWAKA MPYA CHIKUBALI NACHUKUA ELA ENYEWE INGINE NMPEKEA MAMA.

HUKUMU YA ALEXEI NAVALNY KUTOLEWA LEO


Alexei Navalny.
Wakuu wa mahakama Nchini Urusi wanatoa hukumu katika kesi dhidi ya kiongozi mmoja wa upinzani, Alexei Navalny.
Kesi hiyo iliyokuwa isikizwe na kuamuliwa tarehe 15 Januari, sasa itasikizwa leo. Wakili wa Navalny anasema kuwa hatua hiyo imepangwa ili kuwahadaa tu maelfu ya wafuasi wake, waliokuwa wakiandaa mkutano mkubwa jijini Moscow tarehe 15.
Hata hivyo saa chache baada ya tangazo hilo maelfu ya watu waliingia ktika mtandao wa Facebook na kupanga kuwa na mkutano mkubwa siku ya Jumanne.
CHANZO BBC

MOURIHO ALAUMU VYOMBO VYA HABARI NA WAAMUZI


Jose Mourinho 
Meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho anaamini kuwa kuna kampeni zinaendelea kuwashawishi waamuzi kutoa mamuzi tofauti dhidi ya timu yake.
Mourinho amekasirishwa na mwamuzi Anthony Taylor kwa kushindwa kutoa penati katika mchezo dhidi ya Southampton ulomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Kiungo Cesc Fabregas alipewa kadi ya njano baada ya kuanguka katika eneo la hatari la Southampton, kwa kukwatuliwa na Matt Target na kuoneka na kama amemuhadaa mwamuzi kwa kujiangusha.
Baada ya mchezo huo Mourinho alilamika kuwa vyombo vya habari, watangazaji mameneja wa timu zingine wote wanatoa shinikizo kwa waamuzi hivyo anadhani kuna kampeni inaoendelea dhidi ya timu yake.
"Sijui kwa nini kuna kampeni inaendelea dhidi ya timu yangu ila sijali,kila mtu anajua ile ilikua ni penati."
Mourinho anafahamika Zaidi kwa kwa kauli zake tata ambazo amekua akizitoa mbele ya waandishi wa habari.
CHANZO BBC

TIMU NANE ZA TENNIS KUCHUANA TANZANIA


Binti akirudisha majibu mchezoni
Timu kutoka nchi za Burundi, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Shelisheli, Sudan, visiwa vya Comoro zitashindana nchini Tanzania hapo mwakani katika michuano ya tennis ya Afrika kwa watoto chini ya miaka 12, 14 na 16.
Shirikisho la tennis Tanzania (TTA) limesema lipo tayari kwa uwenyeji katika michuano hiyo itakayochezwa kuanzania January 11-19 katika viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam.
Kocha Majuto Majaliwa, anayetambulika na shirikisho la tennis duniani (ITF) amesema wachezaji wa Tanzania wataanza mazoezi Jumamosi ili kujiweka tayari.
“Tumechagua timu yenye wachezaji wazuri ambao wataweza kuipeperusha bendera ya Tanzania nyumbani”.
‘Kuwa wenyeji ni furaha kwetu kwa sababu wachezaji watakuwa wakicheza nyumbani katika viwanja walivyovizoea”, alisema Majaliwa.
Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kuandaa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

ALAN IVIRINE AFUKUZWA KAZI WEST BROM


Alan Ivrine
Timu ya West Brom imemfuta kazi kocha wake Alan Ivrine ambaye amekuwa na klabu hiyo kwa miezi saba tangu apate kibarua hicho.
Kocha huyo mwenye miaka 56 raia wa Scotland alikuwa na mkataba wa miezi 12 ambaa upo katika mfumo wa uendelevu.
Ivrine alichukua nafasi ya Pepe Mel ambaye alikuwa akikinoa kikosi hicho ambapo kwa sasa mfululizo vipigo na hiki cha Jumapili cha 2-0 toka kwa Stoke City kimeuchefua timu hiyo na kuona iko haja kocha huyo kuachia ngazi.
CHANZO BBC

MVUA YASABABISHA MAFURIKO DAR.NA KUSABABISHA WATU WAWILI KUPOTEZA MAISHA

mvua ilionyesha jana kwa muda wa saa mbili imeleta mtafaruku Dar,kupelekea watu wawili kupoteza maisha na mafuriko kukithiri huku Air port nayo maji yaingia ndani.

MAREKANI YATUMA MELI YA KIVITA INDONESIA


Manowari ya Marekani
Wanamaji kutoka Marekani wamesema kuwa wanapeleka moja ya Manowari ya kivita kutafuta ndege ya AirAsia iliyopotea tangu jumapili katika Bahari za Indonesi.
Manowari hiyo ijulikanayo kwa jina la USS Sampson inatarajiwa kufika leo katika eneo la Java Sea today ikiwa ni siku ya tatu tangua kuanza msako dhidi ya ndege hiyo. Idadi ya wataalamu wa kimataifa wanaoitafuta ndege hiyo imeongezeka ambapo kwa sasa nchi za Singapore, Malaysia ,Australia,Korea Kusini,Thailand na China wanashiriki katika kazi hiyo. Mkuu wa Operesheni ya uokoaji na utafutaji ndege hiyo Henry Bambang Soelistyo amesema kwa sasa kuna jumla ya Meli 30,ndege 15 na Helkopita katika eneo la tukio. Ndege hiyo ilipotea ilipokuwa ikisafiri kutoka Surabaya Indonesia kuelekea Singapore ikiwa na abiria 162.
CHANZO BBC.

HATUKUSHAMBULIA RAIA SOMALIA;MAREKANI


Mpiganaji wa Al Shabab
Marekani imesema kuwa bado inatafakari matokeo ya shambulio la anga lililofanyika Kusini mwa Somali kumlenga kiongozi mwandamizi wa kundi la wapiganaji wa Al Shabab.
Ndege za Marekani
Msemaji wa idara ya usalama ya Marekani amesema shambulio la anga katika karibu na eneo la Saakow halikuwa na dalili zozote za kuleta madhara kwa raia na hakuna raia waliodhurika.
Shambulio hilo limetekelezwa siku chache tangu mtu anayedhaniwa kuwa ni mfuasi wa kundi hilo kushambulia kambi ya majeshi ya Somalia na Jeshi la Muungano wa Afrika.
CHANZO BBC.

PICHA ZA GARI LILILOTEKETEA KWA MOTO LEO ZIKO EWANI.

 GARI LILIANZA KUSHIKA MOTO LIKIWA KWENYE ACHA LIFOLENI NDIPO DEREVA ALIPOAMUA   KULIPELEKA PEMBENI NA KURUKA

MESSI KUPEWA TUZO YA HESHIMA


Lionel Messi
Chama cha soka cha Hispania (LFP) kimetangaza kitampa Lionel Messi tuzo ya heshima kwa kuvunja rekodi ya ufungaji bora wa la liga kwa muda wote.
Messi amevunja Rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Telmo Zarra ya kufunga Bao 251 alipofunga mabao matatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Sevilla.
Rais wa chama cha soka cha Hispania Javier Tebas, amethibitisha kuwa watatoa tuzo hiyo kwa mshambuliaji huyo wa timu ya Barcelona.
Messi atapewa Tuzo hiyo Januari 11 katika Uwanjani Nou Camp wakati Barca itakapocheza Mechi ya Atletico Madrid.
Mpaka sasa Messi, amekwisha funga jumla ya mabao 258 katika ligi ya Hispania, huku hasimu wake wa karibu Cristiano Ronaldo akiwa nafasi ya tisa katika historia ya ufungaji bora wa muda wote

NDEGE ILIYOPOTEA KUENDELEA KUTAFUTWA.


Airasia iliotoweka
Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.
Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.

ABIRIA MIAMOJA WAKWAMA;ATC


Shirika la ndege Tanzania ATC
Zaidi ya abiria mia moja wa ndege ya ATC wamekwama nchini Tanzania, baada ya safari zao kuarishwa. Wengi wao wakielekea nchini Comoros na wengine wakiwa katika safari za ndani, kuelekea Mtwara na Kigoma wamekwama kwa siku mbili mjini Dar es salaam.
Abiria hao imebidi wakodiwe hoteli ilivyo ada wakisubiri muafaka wa namna watakavyosafiri kuelekea Comoro. Sharifu Hashim, Balozi wa heshima wa Comoro huko Chicago nchini Marekani, anasema mambo yake mengi yamekwama kutokana na tukio hili na hajapata uhakika ataondoka lini
Zenabal Mwarabu yeye hofu yake ni kwa namna gani ataweza kuiwahi ndege aliyokuwa aunganishe Kisiwani Comoro kuelekea katika kisiwa kingine cha Rarinyo.
Msawi Seifu anasema ijapokuwa tatizo hili limetokea lakini Air Tanzania ni mkombozi kwa wana Comoro….Lily Fungamtama, Mkuu wa Kitengo cha Biashara amesema tayari Air Tanzania inashughulika kuhakikisha abiria wote wanasafiri mapema kesho .
Sikukuu za mwisho wa mwaka ndilo tatizo la kukwama kwa abiria hao,kwani marubani hawajarejea kazini tangu walipoondoka, na walitegemewa kurejea kazini tarehe 27 mwezi huu, baada ya sherehe za Christimas, lakini haikuwa hivyo na kusababisha sintofahamu hiyo.

BALOON YATEKETEA KWA MOTO MAKUMBUSHO

Gari aina ya Baloon limewaka moto na kuteketea kabisa maeneo ya makumbusho hakuna aliyeumia wala kupoteza maisha tukio hilo limetokea sasa hivi
taarifa kamili itakujia baade

BAADA YA MUDA MFUPI MVUA KUKATIKA NAHAYA NDIO YALIYOJIRI NDANI YA DAR NABADO WINGU LIMETANDA

TAHADHARI;MVUA KUBWA DAR INANYESHA,HUENDA IKALETA MADHARA HIVYO TUWE MAKINI.

PATCHO MWAMBA AKANA KUFUMANIWA!


Mwigizaji na mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba ameibuka na kukanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo. Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni aliipost mwenyewe baada ya kupata aleji ya macho ambapo baadaye ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi. "..

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI AFUNGUKA KUHUSU MAFUTA.


Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo bado inayowauzia wananchi wake mafuta kwa bei ya juu licha ya kuwa bei ya mafuta katika soko la dunia kushuka kwa zaidi ya asilimia 50.
Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ameyasema hayo wakati akiongea na Wananchi wa Halmashauri ya mamlaka ya mji mdogo wa Kyela na kusema kuwa kumekuwepo na bei kubwa ya mafuta nchini ikilinganishwa na nchi nyingine.

Jumapili, 28 Desemba 2014

HII NI LAANA,,,,SI BURE.NJEMBA LAJIONGEZA MAKALIO.

BASI LA ZUBERI LAGONGANA USO KWA USO NA COSTA

Basi la Zuberi no 3,limegongana uso kwa uso na costa hakuna alietoka kwenye costa na imekwisha nyang'anyang'a.hali hii imepelekea waliokuwa kwenye gari nyingine kushuka na kuokoa majeruhi.nimbele kidogo ya Singida mjini.

UPEPO WAKWAMISHA UOKOAJI MELI ILIYOZAMA


Meli ya uokoaji 
Waokoaji wamekuwa wakipambana na upepo mkali pamoja na mawimbi ya bahari gizani kuwakoa karibu abiria 300 ambao wamekwama ndani ya ferry moja ya Italia iliyokuwa imeshika moto kwenye bahari ya Adriatic.
Maofisa nchini Italia wanasema kuwa oparesheni ya uokoaji itandelea.Hadi sasa watu 190 wamekolewa kutoka kwa ferry hiyo.
CHANZO BBC

FILAMU YA INTERVIEW YATIKISA MTANDAONI

Filamu ya Interview
Kampuni ya Sony Picutues inasema kuwa - the interview - ambayo ni filamu yenye utata ya dhihaka kuhusu njama ya kumuua kiongozi wa korea kasakzini Kim Jong un imekuwa yenye mafanikio zaidi mtandaoni.
Kampuni hiyo inasema kuwa filamu hiyo imenunuliwa na pia kukodishwa zaidi ya mara milioni mbili kwa muda wa siku nne tangu iwekwe kwenye mitandao.
Sony iliahirisha mpango wake wa filamu baada ya komputa za kampuni hiyo kudaiwa kuingiliwa na wadukuzi,huku Korea Kaskazini ikihusishwa katika udukuzi huo.
CHANZO BBC

NDEGE ILIYOPITEA JANA YAENDELEA KUTAFUTWA


Airasia iliotoweka
Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.
Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.
CHANZO BBC

WATOTO WAZUIWA KUITEMBELEA ISRAELI

Watoto waliotekwa Gaza ndani ya Basi 
Kundi la Hamas limewazuia kundi la watoto kutoka ukanda wa Gaza wengi wakiwa ni wale waliowapoteza wazazi kwenye vita vya hivi majuzi kati ya Hamas na Israel waliotaka kuitembelea Israeli katika ziara ambayo waandalizi wake wanasema ililenga kuleta uwiano. Msemaji wa Hamas anasema kuwa ziara hiyo ilizuiwa ili kulinda tamaduni ya watu wa ukanda wa Gaza.
Wapiganaji wa kundi la Hamas wamezuia kundi la watoto kutoka Gaza wengi wao wakiwa ni wale ambao wazazi wao waliuawa katika vita.
Wanaharakati wa masuala ya Amani waliowasaidia watoto hao kufanya safari hiyo wamesema kuwa mamlaka ya Gaza waliruhusu watoto hao kufanya safari yao lakini wakabadili msimamo wao baadae.
chanzo bbc