Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Ijumaa, 26 Desemba 2014

. MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU

Anaitwa Brian Deacon mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford
Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao.

Ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa naye binti yao aitwaye Lara Deacon, ndoa ya pili alioana na
mwanamama Natalie Bloch mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya AOKOKE mara baada ya kuitazama akiwa na
miaka 30. Alipita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya 1000 ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza
(screen test) kuona kwamba wanafaa.
Brian ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani
na uigizaji.
Kabla ya kuchaguliwa mtihani wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja
moyo kwakumweleza hadhani kama yeye (Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu.
Baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa
kuigiza, sauti yake na mambo mengine, ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo
kutoka kwa muongozaji.
Wiki 3 kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema
kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu
vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.
Katika miezi 7 waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian anasema, walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa 12 za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine
aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini mwenyewe alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza.
Wakati huo wote alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,
siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na
mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.
Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 walikuwa
wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata,cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)
azungumze nao warejee kazini,akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon.
Akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi .
Kiujumla Brian anasema haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia, walikutana na vipingamizi vingi vya kishetani kwani shetani hakupenda filamu hiyo irekodiwe.
Baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18, filamu ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu huko Marekani, na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona jinsi filamu hiyo
ilivyonanguvu, ukweli na kugusa mioyo ya watu na akaamua kuokoka.
Kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni 3 katika nchi 233, zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao
na kumpokea Yesu.
Brian ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine wanavyojua hivyo. Mara nyingine watu
waliosema wamemwona Yesu katika maono huwa wanaona sura ya Brian. THANK BE GOD
UONGOZI WA rayshughuli.blogspot.com UNAPENDA KUWATAKIA SKUKUU NJEMA.NA MUNGU AWE PAMOJA NANYI.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni