Mji wa Cape Town, Afrika kusini
Mfumo wa kutambua matumizi ya risasi
ujulikanao kama Shot Spotter umeonyesha matumaini katika kupambana na
uhalifu, Afrika Kusini.
Mfumo huo unawajulisha polisi kwa kupitia
ujumbe mfupi wakati wowote ambapo kundi moja wapo litakuwa limetumia
risasi katika eneo la Hanover Park.Majengo ya Cape ni maarufu kwa vurugu za magenge na biashara ya madawa ya kulevya.Eneo hili lina idadi kubwa ya mauaji duniani kote.
Kuna mamia ya majengo ambayo yameshikana huku wakazi wake wakiishi maisha duni yasiyo na ajira.
Katika eneo hili pekee la Hanover Park, magenge ishirini yanashindania eneo hili ambalo maelfu ya watu wanaliita ndio nyumbani.
Wakati mwengine kunakuwa na upigaji risasi wa makusudi, lakini wakati mwengine pia watu hujikuta katika hali ya vurugu kwa bahati mbaya.
Katika siku za hivi karibuni, teknologia imeanza kutumika. Vinasa sauti katika eneo hilo vimeunganishwa na mfumo wa GPS ambapo kunapokuwepo tu kwa upigaji risasi, mfumo huo unawaajulisha polisi na mradi wa kusitisha mapigano katika hatua za mwanzo za vurugu.
Teknologia hii ndio imeanzishwa lakini imesaidia kupunguza mauaji na vile vile imesaidia polisi kuwepo katika matukio pindi yanapotokea. Watu hapa wanasema, ikiwa mfumo huu unaweza kuokoa maisha ya mtu mmoja pekee, basi kuna kila sababu ya kuwekeza.
chanzo bbc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni