Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 24 Desemba 2014

ALIYEKUWA RAIS WA MAREKANI ALAZWA


George H.W Bush
Aliyekuwa rais wa Marekani George H.W Bush amekimbizwa katika hospitali moja ya Houston nchini Marekani baada ya kupatikana na tatizo la kupumua.
Kulingana na madaktari,Bush mwenye umri wa miaka 90 anachunguzwa katika hospitali ya Methodist.
Alipelekwa katika hospitali hiyo na ambalensi jumanne usiku.
Wawakilishi wa Bush wanasema kuwa hatua hiyo ya kupelekwa hospitali ni kama tahadhari.
Rais huyo wa 41 ndio mzee kuwahi kuiongoza Marekani akimshinda Jimmy Carter kwa miezi michache.
Alihudumu kwa muhula mmoja baada ya kushindwa na Rais Bill Clinton.
Bush ambaye hawezi kutumia miguu yake,hivi majuzi alionekana amekaa katika kiti cha magurudumo katika hafla iliofanyika mwezi November katika chuo kikuu cha Texas na mwanawe aliyekuwa rais George W Bush
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni