Ndugu wa abaria waliopotea kwenye ndege ya AirAsia wakilia kwa uchungu
Hali mbaya ya hewa imechelewesha
zoezi la anga na majini la utafutaji wa ndege ya AirAsia aliyoanguka
ikiwa na watu 162 baada ya kuwepo kwa dhoruba katika pwani ya eneo la
Borneo siku ya jumapili.
Kufuatia kupatikana kwa vipande vya
mabaki ya ndege hiyo siku ya jumannne, kiongozi wa taasisi ya uokoaji na
utafutaji amesema miili mitatu imepatikana hadi sasa kutoka katika eneo
la bahari ya Java.Wapiga mbizi wa kikosi cha maji cha jeshi wanatarajiwa kuanza kutafuta miili na kinasa sauti cha ndege hiyo katika kina cha chini cha maji katika eneo linalosadikiwa ndipo ndege hiyo ilipoangukia.
Ndege hiyo ilipotea ikiwa safarini ikitokea mji wa Surabaya nchini Indonesia kuelekea nchini Singapore.
chanzo bbc.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni