Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumapili, 21 Desemba 2014

US YITAKA K.KAKSKAZINI KUILIPA SONY


Wakuu wa kampuni ya filamu ya Sony Pictures.Marekani imeitaka Korea Kazkazini kuilipa kampuni hiyo kwa hasara iliopata baada ya madai ya kuhusika na uhalifu wa mtandao dhidi yake 

Marekani imezitaka China na nchi zingine kuthibitisha kuwa Korea Kaskazini ilihusika na uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony Pictures.
Marekani inasema kuwa Korea Kaskazini ni lazima ikiri kuwa ilihusika na iilipe Kampuni ya Sony kutokana na hasara ambayo imepata
Korea Kaskazini imeyataja madai hayo ya Marekani kuwa ya uongo.
Wataalamu wanasema kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa Korea Kaskazini ilihusika.
Lakini mwandishi wa BBC nchini Korea Kusini anasema kuwa kampuni ya Sony Pictures nchini Marekani na wakuu wake nchini Japan watahitajika kuamua iwapo wataonyesha filamu ya uchesi yenye utata ya rais wa Korea Kazkazini Kim Jong-un.
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni