Michael Van Gerwen
Mchezaji wa mchezo wa Vishale
Michael van Gerwen,amefanikiwa kuingia hatua ya nane bora katika michezo
ya dunia kwa kumfunga Terry Jenkins kwa mabao 4-1
Katika michezo
mingine Robert Thornton pia aliibuka kidedea kwa kumchapa Benito van de
Pas kwa mabao 4-0 na atachuana na Van Gerwen katika hatua ya robo
fainali.Raymond van Barneveld alifanikiwa kuingia robo kwa kupata ushindi wa 4-3 dhidi ya mpinzani wake Jamie Caven.
Huku Stephen Bunting akishinda kwa ushindi wa 4-1 mbele ya James Wade, Mwingereza Smith alipata ushindi licha ya kutanguliwa kwa 2-0 kwenye awamu ya kwanza na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Brendan Dolan.
Mchezaji wa Uholanzi Vincent van der Voort alimaliza kwa kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 kwa kumtwanga Max Hopp toka Ujerumani.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni