Ripoti kutoka Gambia zinasema kuwa
rais Yahya Jammeh amerudi nchini humo kutoka ziara ya ughaibuni kufuatia
njama ya kutaka kumpindua.
Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.Haijulikani ni wapi rais Jammeh alikokuwa huku ripoti zikidai kuwa alikuwa nchini Ufaransa na wengine wakisema alikuwa Dubai.
Mkuu wake wa itifaki ameiambia BBC kwamba kila kitu kiko shwari katika mji mkuu.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni