Shughuli za upigaji kura
zinaendelea nchini Liberia kuwachagua maseneta wapya licha ya kuwepo kwa
hofu kwamba kura hiyo huenda ikachangia kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.
Uchaguzi
huo umehairishwa mara kadha lakini rais Ellen Johnson - Sirleaf anasema
kuwa kura hiyo ni lazima ifanyike wakati huu ili kuzuia msukosuko .Mikutano ya kisiasa ilipigwa marufuku kufuatia hatari iliyotokana na ugonjwa wa ebola ambao umewaua maelfu ya watu magharibi mwa afrika.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa watu wengi nchini Liberia wanaamini kuwa kura hiyo ni hatari sana na kesi ya kuizuia isifanyike imepelekwa kwenye mahakama ya juu.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni