Manowari ya Marekani
Wanamaji kutoka Marekani wamesema
kuwa wanapeleka moja ya Manowari ya kivita kutafuta ndege ya AirAsia
iliyopotea tangu jumapili katika Bahari za Indonesi.
Manowari hiyo
ijulikanayo kwa jina la USS Sampson inatarajiwa kufika leo katika eneo
la Java Sea today ikiwa ni siku ya tatu tangua kuanza msako dhidi ya
ndege hiyo. Idadi ya wataalamu wa kimataifa wanaoitafuta ndege hiyo
imeongezeka ambapo kwa sasa nchi za Singapore, Malaysia ,Australia,Korea
Kusini,Thailand na China wanashiriki katika kazi hiyo. Mkuu wa
Operesheni ya uokoaji na utafutaji ndege hiyo Henry Bambang Soelistyo
amesema kwa sasa kuna jumla ya Meli 30,ndege 15 na Helkopita katika eneo
la tukio. Ndege hiyo ilipotea ilipokuwa ikisafiri kutoka Surabaya
Indonesia kuelekea Singapore ikiwa na abiria 162.CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni