Waziri mkuu mpya wa Somali Omar Sharmarke
Bunge la Somalia limeidhinisha
uteuzi wa waziri mkuu mpya akiwa ni afisa wa tatu kuhudumu katika wadhfa
huo katika kipindi cha miaka miwili.
Wengi wa wabunge walimpigia kura Omar Ali Sharmarke.Mapema mwezi huu walipitisha mswada wa kutokuwa na imani dhidi ya aliyekuwa waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed,baada ya majaribio matatu ya kutaka kumuondoa madarakani kuambuliwa patupu.
Waandishi wanasema kuwa serikali ililemazwa na vita villivyokuwa kati ya wafuasi wa Abdiweli dhidi ya wale wanaoumuunga mkono rais Hassan Sheikh Mohamud.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni