Idadi ndogo ya wapiga kura imeripotiwa kwenye kura ya kuwachagua maseneta nchini Liberia.
Kura
hiyo ilikuwa imeahirishwa mara mbili kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa
ebola na huenda hofu ya ugojwa huo iliosababisha watu kukosa kufika kwa
vituo vya kupigia kura.Wapiga kura walishauriwa kusimama umbali wa mita moja kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine walipokuwa wakipanga milolongo kupiga kura baada ya viwango vyao vya joto kuchukuliwa na maafisa wa afya.
Kwenye taifa jirani la Guinea waandamanaji waliwazuia wafanyikazi wa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF kuweka kituo cha ebola kusini mwa nchi hiyo.
Polisi wanasema kuwa mahema yalichomwa na wafanyikazi wakafukuzwa na megenge ya vijana.
Jamii kwenye sehemu zingine za magharibi mwa afrika zilipinga jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo zikihofia kuwa huenda zikapata maambukizi kutoka kwa wafanyikazi wa kutoa huduma za afya.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni