Makamo wa rais wa Kenya, William
Ruto, anasema kuwa askari wa usalama wa Kenya wamewaandama wapiganaji wa
al-Shabaab hadi kwenye kambi yao nchini Somalia, baada ya shambulio
dhidi ya basi kaskazini-mashariki mwa Kenya hapo jana ambapo raia 28
waliuliwa.
Bwana Ruto alisema wapiganaji zaidi ya 100 waliuliwa katika operesheni mbili tofauti.Alisema kambi ya al-Shabaab iliangamizwa.
Habari hizo hazikuthibitishwa na upande wa pili.
Gavana wa Mandera - ambako shambulio la jana lilitokea - amelaumu vikosi vya usalama kwa kushindwa kuwalinda raia.
Alisema polisi kawaida wanashindwa kufanya uchunguzi kamili baada ya mashambulio.
chanzo BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni