Kikao cha wabunge wa Somali Chatibuka
mjini Mogadishu.kikao hicho kilitarajiwa kujadili hatma ya waziri mkuu
Abdiweli Sheikh Ahmed
Kwa mara ya pili katika kipindi cha
juma moja ,kikao cha wabunge wa Somali kilichoitishwa ili kuijadili
hatma ya waziri mkuu nchini humo kimeisha kwa kelele na ghasia.
Wabunge
walitarajiwa kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu Abdiweli
Sheikh Ahmed ,lakini wafuasi wake walikataa kukaa na kuanza kuimba na
kubeba mabango.Bunge la Somali limelemazwa na mgogoro uliopo kati ya waziri mkuu na rais Hassan Sheikh Mhamud.
Marekani imesema kuwa kura hiyo ya kutokuwa na imani haina maslahi ya raia.
Umoja wa mataifa nao umesema kuwa una wasiwasi kuhusu ufisadi wa ununuzi wa kura unaokabili kura hiyo.
chanzo BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni