Shule
![Shule](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhowosffr85R15Iy8OeXGODZp5kd2v0ncDhKEPBKYhYhAU1s6Cjj7sf6d6qCwYkz-nRr7mMc1AtErm869z7-WhD5IUWXoPH-MEepRv9S3MAMZ_7sKHSvmJEdFmwxh2vFgslpN7fTH_kULGM/s1600/Tangazo.jpg)
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache
Alhamisi, 27 Novemba 2014
TUNDU LISSU AMEFUNGUKA BUNGENI NA AMESEMA MH.MUHONGO AMESEMA UONGO
Lissu: Naomba niseme kuwa Bunge lako limepotoshwa moja kwa moja na Mh. Muhongo
Lissu: Kiambatanisho namba 2 sio ushahidi wa standard charted Hong Kong kutambua chochote ila ni hati ya madai.
Lissu: Vitambulisho viwili alivyoleta Muhongo ni kesi za mahakama kuu za mwaka huu, hazina ushahidi wowote wa tuhuma zake
Lissu: Kwa ushahidi wa taarifa ya kamati na CAG hizi ni pesa za umma, kama zisingekuwa za umma Rais asingeelekeza zilipwe
Lissu: Inakuwaje pesa za binafsi zitolewe maamuzi na Rais, Mawaziri, na Magavana?
Lissu: PAP waweze kupewa hizi pesa ilibidi wapewe kibali na Waziri Muhongo, lakini haijapata usajili hivyo si kampuni halali.
Lissu: Ndani ya siku moja zimetoka bilioni 78, na kama fedha zinazodaiwa ni binafsi kwanini wapewe Viongozi wa Umma na dini?
Lissu: Kuna ushahidi wa kutosha unaothibitisha kuwa hizi ni fedha za umma. TRA, TAKUKURU na CAG wamekiri ni fedha za umma
Lissu: Rushwa tupu imetambaa hadi mahakamani, Majaji wanapewa fedha tukiuliza mnasema ahahahha.
Lissu: Waziri Mkuu, Tibaijuka , Muhongo na wote waliotajwa walioko humu ndani, tuanze nao maana hawa tunawaweza
Lissu:Kuna la kusisitizwa hapa kuhusu BOT,Benki kuu ni huru na haiwezi ikajificha nyuma ya ushauri mbovu wa Mwanasheria mkuu.
Lissu: TRA pekee ndio chombo kikuu chenye mamlaka hapa nchini kutoa ushauri juu ya ushuru upi wa kodi ulipwe
Lissu: Mwanasheria Mkuu sio mshauri mkuu wa maswala ya kodi hapa nchini ila TRA.
Lissu: Kamati inasema Waziri Mkuu awajibike kwakuwa ndiye mwajibikaji mkuu wa shughuli za serikali, hii ni sahihi kabisa.
Lissu: Tunamwachaje Waziri wa wizara ya fedha ambaye ndiye mhusika mkuu wa masuala ya fedha?
Lissu: Mkuu wa Kitengo cha Financial Intelligence Unit ndani ya Wizara ya Fedha anatakiwa kuwajibika
Lissu: Leo yametokea yaliyozungumzwa toka mwaka 1994 kuwa IPTL itakuja kutuumiza
Lissu: Tunataka fedha zetu zirudi maana leo haya yanatokea Jakaya Kikwete ndiye Rais wa nchi
Lissu: Wakati IPTL inakuja, Rais Kikwete alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, wakati wanasaini mkataba alikuwa Waziri wa Fedha
Lissu: Hakuna jambo baya kama Hakimu kupewa milioni 400, na hiyo sio dhihaka ila ni wajibu wetu kuyasema haya
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni