Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatatu, 17 Novemba 2014

UNAHITAJI PENZI LENU LIENDELEE KUCHANUA KILA MARA .

Ipo sababu moja inayowafanya watu kuoana. Aidha, vipo vitu vingine vingi ambavyo hutengeneza dhamira ya wawili kuingia safarini kuelekea katika ndoa.

Kimojawapo ni hali isiyo na wasiwasi, yaani kuwa katika pointi kwamba hakuna cha kungoja wala kupoteza kuingia kwenye ndoa. Picha ya wazi inajionesha kuwa uliyenaye atakupa unafuu wa kimaisha, baada ya hapo mapenzi yanafuata.

Wataalamu wa saikolojia wanaelekeza kuwa ndoa kama gari, basi mapenzi yanaweza kukaa siti ya nyuma. Siti za mbele vitakuwepo vitu ambavyo vinaleta maana ya wawili kuoana.

Ndoa nyingi zinafungwa kwa kuzingatia mapenzi, mvuto na tamaa. Hata hivyo, mara nyingi upendo wa mwanzoni hubadilika kuwa msamiati ndani ya nyumba nyingi kadiri wanandoa wanavyokaa kwa muda mrefu.

Wengi katika ndoa mpya huwa kama nusu pepo ambayo hugeuka kuwa migogoro na hata chuki. Hii ndiyo sababu siku hizi kuna ndoa nyingi ambazo wenzetu Ulaya huziita hollywood, yaani zipo zipo na hudumu kwa muda mfupi.

Hii inamaana kuwa hollywood ni ndoa zenye nakshi nyingi za kimapenzi mwanzoni lakini baada ya muda upendo hutoweka. Mume na mke kila mtu kivyake. Watatengeneza wenzi wa pembeni na baada ya chuki kuzidi, huachana baada ya kipindi kifupi!

Kuna watu ambao kutokana na matatizo hayo huamua kuwekana kinyumba au kwa lugha rahisi ni kuishi bila kufunga ndoa. Hii ndiyo sababu ya kutoa somo hili ili kuwajenga wanandoa, wawe na uelewa wa kutosha wa kudumisha mapenzi.

Stadi wa masuala ya kimapenzi ni wengi, wanapatikana kwenye magazeti, majarida, televisheni, intaneti na kadhalika. Muhimu kwako ni kujua jinsi ya kudumisha uhusiano wako, ujae mapenzi kwa maisha yenu yote.

Hapa chini kuna vitu vya kufanya;
Kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni kuwa unawajibika katika mapenzi ndani ya ndoa yako. Hii inamaana kwamba ni wewe pekee unayepaswa kuyafanya mapenzi yawepo kwenye nyumba yenu.
Wanandoa wengi hasa vijana hawalikubali hili, wanaongozwa na mfumo wa jino kwa jino. Hawataki kujishusha! Wakati unasoma hapa ni vema ukaelewa kwamba hiyo si njia sahihi ya kuishi ni lazima uoneshe mapenzi ili nawe upendwe.

Siku zote mapenzi hupimwa na vitu vizuri ambavyo unavifanya kwa mwenzi wako. Uungwana, wema na ukarimu ni mambo ambayo unapaswa kuyafanya kwa lengo la kuifanya ndoa yako iwe na afya. Kinyume chake, unaiweka mtegoni.
Kisaikolojia ni ngumu kuwa muungwana au kuonesha ukarimu kwenye matatizo. Mpenzi wako amekuudhi, hapo ni ngumu kuepeka hasira. Hata hivyo, ukiwa ndani ya ndoa ni vizuri ukajifunza jinsi ya kutatua migogoro ya kimapenzi.

Umegombana na mpenzi wako, hamtakiwi kufunikwa na mgogoro katika mambo yenu yote. Ni lazima muyaweke mezani na myatatue. Kila mmoja anatakiwa awe na fikra zilizo wazi, pia moyo wa kusahau. Migogoro yote ya ndoa inatatuliwa ikiwa wote mtakuwa radhi ya kuidumisha.
Ukiwa kwenye ndoa, chukulia mtu wa tatu (msuluhishi) kazi yake ni kuonesha tofauti zenu na kutoa njia za kumaliza tatizo. Haji kusuluhisha mgogoro wenu. Suluhu itapatikana ikiwa ninyi wenyewe wawili mtakuwa mmeamua kumaliza tofauti zenu.

Lipo tatizo moja kubwa ambalo limetuama kwenye fikra za wanandoa wengi. Hii ni ukweli kwamba wapenzi wengi baada ya kuishi kwa muda mrefu ndani ya ndoa huishiwa na hisia za kimapenzi.
Kitu muhimu kwako ni kuondoa fikra hizo na ukubaliane na ukweli halisi kwamba upendo unaouonesha umefichwa ndani ya moyo wako. Yaache wazi kwa mpenzi wako ili mfurahi pamoja; hauwezi kujuta.

Nimeeleza hapo kabla kwamba ili upendwe inabidi kwanza wewe mwenyewe uoneshe mapenzi. Migogoro ndani ya ndoa itatatuliwa iwapo wanandoa watakuwa na dhamira ya kumaliza tofauti zao. Ni lazima kila mmoja akajua thamani ya ndoa yake.

Hata hivyo, ipo kachumbari ya mapenzi, hii ni chachandu ambayo ikizingatiwa ndoa nyingi zitadumu, hazitoathiriwa na migogoro,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni