Thuluthi moja ya wahanga wa biashara ya
kusafirisha binaadamu kwa magendo ni watoto na
idadi yao kwa jumla imekuwa ikizidi
kuongezeka.Ripoti iliyotolewa leo hii na Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Madawa ya
Kulevya na Uhalifu (UNODC) na kuhusisha kipindi
cha mwaka 2010 hadi 2012 imekadiria kwamba
wahanga wote wa biashara ya kusafirisha
binaadamu waliogundulika walikuwa na umri mdogo.
Kiwango hicho ni asilimia tano zaidi kuliko ilivyokuwa
kati ya mwaka 2007 na 2010. Tatizo hilo ni sugu
zaidi barani Afrika na Mashariki ya Kati ambapo
wengi wa watu wanaosafirishwa kwa magendo ni
wavulana na wasichana, ingawa kwa ujumla uhalifu
huo hufanyika dunia nzima. Shirika hilo la UNODC
limekusanya taarifa kutoka takribani mataifa 152
ambako wahanga wamelazimishwa kuingia kwenye
kazi za ngono, vibaruwa vigumu na shughuli
nyenginezo. Wanaofanya biashara hiyo ya
kusafirisha binaadamu mara nyingi huwaandama
wanawake na wasichana.
CHANZO DW.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni