Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumanne, 18 Novemba 2014

KOREA YA KASKAZINI KUFIKISHWA ICC


 Viongozi wa Korea Kaskazini
Baraza la umoja wa mataifa la haki za binadamu limesema Korea Kaskazini inastahili kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu kutokana na kukiuka haki za binadamu.
Katika baraza hilo zimetolewa tuhuma dhidi ya Korea Kaskazini kwamba serikali yake imekuwa ikifanya vitendo vya ukiukaji haki za binadamu.
Mapendekezo hayo yaliyopitishwa na baraza la haki za binadamu la kimataifa yanapaswa kupigiwa kura ili kupitishwa na bunge yaweze kuhalalishwa.
Ripoti ya mwezi Februari mwaka huu iliyotolewa na umoja wa mataifa ilibainisha kuwa watu wa Kawaida Korea Kaskazini wanakabiliawa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na pia mauaji.
Umoja wa mataifa unafanya uchunguzi dhidi ya Korea Kaskazini ili kupata ushahidi wa majina ambayo yapo kwamba taifa hilo limeua, likitesa watu,ukatili wa kisiasa na uhalifu mwingine.
Hata hivyo China na Urusi wanaoshikilia kura ya Veto katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,wamepingana na mapendekezo hayo ya Baraza la Usalama, huku nayo Korea Kaskazini ikiipinga ripoti hiyo.
Wanadiplomasia wana wasiwasi kuwa huenda China inataka kutumia kura yake ya Veto kupinga Baraza la Usalama kupeleka kesi zake katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.
CHANZO BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni