Chuck Hagel,waziri wa ulinzi mstaafu wa Marekani
Afisa mwandamizi wa serikali ya Marekani amesema waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Chuck Hagel anajiuzulu katika baraza la mawaziri la Rais Barack Obama.
Hagel ambaye ni seneta wa zamani wa chama cha Republican alikuwa waziri wa ulinzi wa Marekani tokea mapema mwaka 2013. Obama anatarajiwa kutangaza kujiuzulu kwa waziri huyo leo hii. Afisa wa serikali aliyetowa habari hizo amekataa kutajwa jina lake kwa sababu haruhusiwi kuzungumzia suala hilo hadharani kabla ya Rais Obama kutangaza rasmi.
chanzo dw
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni