Shirika la ulinzi la ulaya,limearifu
kwamba mabaki ya ndege ya shirika la ndege la Malaysia yaliyookotwa
huko mashariki mwa Ukraine hatimaye yanarejeshwa Uholanzi.
Mkuu wa
shirika hilo Michael Bociurkiw ameiambia BBC mabaki yaliyokusanywa na
timu ya uchunguzi kutoka Ujerumani, ambao wamekwisha ingia katika ardhi
inayo dhibitiwa na serikali ya Ukraine na mabaki hayo yatasafirishwa kwa
ndege kutoka katika mji wa Kharkiv.Timu hiyo ya watafiti wa Kijerumani inaongoza timu ya watafiti wa kimataifa kufuatia ajali hiyo ya ndege iliyotokea mwezi July kutokana na maombi maalumu ya serikali ya Ukraine.
Ndege hiyo iliondoka katika uwanja wa Amsterdam na idadi kubwa kati ya abiria 298 ya waathirika wa tukio hilo ni Wajerumani .
Juhudi za uchunguzi huo zinakwamishwa na mgogoro unaoendelea huko Mashariki mwa Ukraine kati ya Urusi na nchi hiyo mgogoro ambao unaungwa mkono na askari wa majeshi ya nchi hiyo.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni