Inawezekana ukawa ni mke wa mtu au una
mpenzi wako ambaye mna matarajio ya kufunga ndoa na kuishi pamoja. Kuna wakati
unaweza kujaribiwa na kujikuta ukikabiliwa na hatari ya kumsaliti mpenzi wako.
Kujaribiwa huko kunaweza kukutokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na
maeneo yako ya kazi au mahali unapofanyia shughuli zako za kila siku. Kwa mfano
inaweza ikatokea umefahamiana na mwanaume mahali pako pa kazi, anaweza kuwa ni
mteja au mfanyakazi mwenzio. Inatokea siku moja anakualika kwa ajili ya chakula
cha mchana, baada ya mtoko huo, unajisikia kutoka naye kwa mara nyingine…………………
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOYmDtUTZF7LVC_ObI_jSY2IUZIJ14d2_D5NLEhTe1LqkQiJx7M-ZLKPa4Q3EiOrBQDZrmlwFBc7R7tigFB_cHCwR1PQpc_0mkkNnzjSucpMC-2YpplAIP-ueyW-a4AFyc3Uh9AISAtYR1/s1600/984238_1076605889020495_5275129449488354061_n.jpg)
Kuna kitu wenzetu wazungu wanakiita Emotional infidelity, kwa tafsiri yangu naweza kusema ni hisia za usaliti katika mapenzi. Maana yake ni kwamba unaruhusu mtu mwingine wa jinsi tofauti azibe pengo la hisia ambalo lingetakiwa lizibwe na mpenzi wako au mume wako. Kama inavyofahamika kwamba wanawake ni viumbe wa hisia, wanapenda sana kusikilizwa, na wanapenda kuona wapenzi wao au waume wao wanawasikiliza. Inapotokea hitaji hilo halitekelezwi na mpenzi au mume wake, basi ni rahisi sana atakapotokea mtu mwingine ambaye bila kujua akamudu kuziba pengo hilo kuvutiwa naye na kuhitaji kuwa naye karibu mara kwa mara.
Hapa chini nitazitaja dalili ambazo zitakuonyesha kwamba ukaribu wako na huyo rafiki utakupelekea kuisaliti ndoa yako:
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiEhZmUtCWDX6uo4u2U8xpnCkd8dOcY2WzI60RGJ6Uwpg6WFg5Ifx6ndYsgNXKHElq4fMkbqn7F2q9qDnneQwQVq44SM8GR3SpcbYZzKiKORBXX5zatwsclA4X6RQ-6BtHYFXYBGr_dY9tB/s1600/mahaba-web.jpg)
1. Unatamani sana kumuona ukiwa na shauku kubwa ya kuwa naye karibu na kutumia muda mwingi kuwa naye
2. Unajikuta ukichagua mavazi na kujikagua sana ukijiuliza jinsi atakavyo vutiwa na mavazi yako pale atakapokuona
3. Unapokuwa naye unajikuta ukimweleza matatizo ya mahusiano yako na mpenzi wako au mumeo
4. Unajikuta ukimgusa gusa wakati mkiongea au kufanya naye utani unaoweza kupeleka ujumbe tofauti kwake kwamba labda umevutiwa naye kimapenzi.
5. Unawsiliana naye kwanza kabla ya kuwasiliana na mpenzi wako au mumeo pale unapokabiliwa na jambo lolote lenye kutatiza na linalohitaji msaada wa haraka au ushauri
6. Unajikuta ukiwaza jinsi gani ungekuwa na amani iwapo ungekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi au ndoa
7. Inawezekana ukawa unamzuingumzia sana kwa mwenzi wako au kwa marafiki zako, au inawezekana ukawa humzungumzii kabisaaa na kuficha urafiki wenu.
8. Unajitahidi sana kuficha urafiki wenu na kutomzunguimzia rafiki huyo kwa mwenzi wako kwa sababu unajua kwamba jambo hilo linaweza kukuletea balaa.
Kwa ujumla unapojikuta umempata rafiki mwenye jinsia tofauti na yako halafu ukahisi kulipukwa na moyo juu yake zikiwemo dalili nilizozitaja hapo juu, basi ujue uhusiano wako na mume au mpenzi wako uko mashakani. Usipokuwa makini utamsaliti.
MC.RAY
WHATSAPP 0659/375263
INSTAGRAM MC.RAYMONDMUSHI
FACE BOOK Raymond Mushi
PAGE Rayshughuli
WHATSAPP 0659/375263
INSTAGRAM MC.RAYMONDMUSHI
FACE BOOK Raymond Mushi
PAGE Rayshughuli
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni