Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis amelitaka bara la Ulaya kutayarisha sera moja na ya haki katika suala la uhamiaji, akisema mamia kwa maelfu ya wahamiaji wanaowasili katika mataifa hayo kila mwaka kupitia baharini wanahitaji kukubalika na msaada, na sio kuwa na sera zenye maslahi binafsi ambazo zinahatarisha maisha na kuchochea mzozo wa kijamii.
Papa Francis ametoa matamshi hayo katika bunge la Ulaya wakati wa ziara fupi iliyokuwa na lengo la kuelezea mtazamo wake kwa Ulaya robo karne baada ya Papa John Paul wa pili kuzuru Strasbourg na kulihutubia bara ambalo bado limegawanywa na pazia la chuma.
Papa Francis amesema anataka kuleta ujumbe wa matumaini kwa watu wa bara la Ulaya ambao hawaziamini taasisi zao , zinazolemewa na mzozo wa kiuchumi na zikiwa mbali na mtazamo wa kiroho katika utamaduni ambao amesema hauthamini tena maadili ya hadhi ya binadamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni