Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumamosi, 29 Novemba 2014

BINTI WA KAZI ALIEMPIGA MTOTO,AVUNJA UKIMYA




Baada ya story ya yule msichana kwa anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya Kimataifa Duniani, leo kipo ambacho amekizungumza kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo.
Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe ambaye kwa sasa amekamatwa na Polisi amesema sababu iliyomfanya amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.
Amesema anajiona mwenye hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo akimpiga kama njia ya kumkanya.
Jolly amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga sana na kutaka kumpiga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni