![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRfBYbGLegoiS9oKTtc3-zv8skotQbn9Tx7870Ndj-uHudyO1Wf2GmfTnmmWNtCMShu92-oMT9Wkfo2PGaeXdi3WZUjxZsPctvbkzQyExcoYJVhpVOjyVV49-ftGOb2AOyJxck7rvWqMHE/s1600/10609452_817949914915095_3904651863143011598_n.jpg)
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, James Mhanusi,ambapo mbali na kuwatia hatiani washitakiwa hao Mahakama hiyo pia imemuachia huru mshtakiwa mmoja kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuna ushahidi unaomhusisha na tukio moja kwa moja,watuhumiwa hao ni James, Elinazi Mshana,Lusajo Jeremia na Abdalah Mohamed ambao kwa pamoja walitenda kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha Oktoba 7, 2013
Mwendesha mashtaka huyo alisema watuhumiwa hao wenye kesi namba 23/2014 walitenda kosa hilo kinyume cha kifungu cha 287 (a) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambapo walifanikiwa kupora Kahawa yenye thamani ya shilingi Milioni 119.2 yenye uzito wa kilogramu 30091.
Akisoma Hukumu kwa watuhumiwa hao, Hakimu Mhanusi amesema kutokana na ushahidi wa upande wa mashtaka na upande wa utetezi mahakama imeona mshtakiwa namba tatu katika kesi hiyo ambaye ni Gwantwa Malakasuka hakukuwa na ushahidi unaomtia hatiani pasipo shaka hivyo akaamuru kuachiwa huru.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni