Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumamosi, 29 Novemba 2014

WALIOKUFA KWA EBOLA WAFIKIA 7,000 SASA.

 Guinea

Takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO, zinaonesha kuwa watu karibu 7,000 wamefariki hadi sasa kutokana na Ebola, karibu wote Afrika Magharibi.
Hao ni watu zaidi ya elfu moja kuliko idadi iliyotangazwa na WHO Jumatano tu.
Vifo vingi zaidi vimesajiliwa Liberia.
WHO inasema watu zaidi ya 16,000 wameugua Ebola hadi sasa.
Waandishi wa habari wanasema kuongezeka kwa idadi ya waliokufa siyo lazima inamaanisha ugonjwa unazidi kutapakaa kwa kasi kwa sababu takwimu nyengine ni za zamani.
Na Rais Francois Hollande wa Ufaransa amezuru Guinea, kiongozi wa kwanza asiyekuwa Muafrika kuzuru moja kati ya nchi tatu za Afrika Magharibi zilizoathirika sana na Ebola.
Bwana Hollande alisema alitaka kuleta ujumbe wa matumaini kwa watu wa Guinea:
"Ufaransa inaweka mfano - tumefanya hivyo kifedha kwa kutoa dola 125 milioni.
Lakini mbali ya msaada wa mali, utu ndio muhimu zaidi.
Na Guinea inapochukua hatua za kuuguza na kuzuwia Ebola isisambae, hivyo inasaidia ulimwengu, Ulaya pamoja na Ufaransa zisije nazo zikapata virusi hivyo vibaya.
Kwa hivyo tuko nanyi katika mapambano haya, vita hivi.
Na ni muhimu kuwa miaka 15 baada ya rais wa mwisho wa Ufaransa kuzuru Guinea, kuwa nami niko hapa kuonesha urafiki, umoja na matumaini."
Rais Alpha Conde wa Guinea alisema Rais Hollande amefika wakati mzuri ili kuonesha kuwa mtu yoyote anaweza kuzuru Guinea.
CHANZO BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni